DRC-CORONA-AFYA

DRC: Kivu Kaskazini inakuwa mkoa wa tatu ambao umeathiriwa zaidi na Corona

Wafanyakazi wa Wizara ya Afya nchini DRC wawakihifadhi nguo zao maalumu baada ya kufanya vipimo vya Corona huko Goma, Kivu Kaskazini.
Wafanyakazi wa Wizara ya Afya nchini DRC wawakihifadhi nguo zao maalumu baada ya kufanya vipimo vya Corona huko Goma, Kivu Kaskazini. ALEXIS HUGUET / AFP

Kivu Kaskazini umethibitishwa kwa mkoa wa tatu ulioathirika zaidi na Covid-19 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya mikoa ya Kinshasa na Kongo Central.

Matangazo ya kibiashara

Tangu mwanzoni mwa mwezi Agosti, kesi 15 za maambukizi ya virusi vya Corona zimekuwa zikirekodiwa kwa siku, na, kulingana na Waziri wa Afya katika mkoa huo, sasa wagonjwa 210 wanaendelea kuhudumiwa katika mkoa wa Livu Kaskazini.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu jijini Kinshasa, Kamanda wa Kamanda Muzembe ongezeko la visa vya maambukizi lilianza kushuhudiwa tangu mwezi wa Julai katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Kulingana na mamlaka ya afya katika mkoa huo, hadi Jumapili, jumla ya wagonjwa 524 wamerekodiwa tangu kupatikana kwa mgonjwa wa kwanza dhidi ya wagonjwa 112 hadi Juni 30. Kwa jumla, wagonjwa 233 walipona, na 77 wamefariki dunia, ikiwa ni pamoja na wawili katika waliofariki dunia vituo vya matibabu ya Covid-19, ameeleza Waziri wa Afya katika mkoa wa Kivu Kaskazini, Daktari Moïse Kanyere.

Kulingana na mamlaka ya afya, mlipuko huo unaripotiwa katika miji mitatu ya mkoa: Goma, Beni na Butembo na katika wilaya tano kati ya sita za mkoa wa Kivu Kaskazini. Kulingana na timu inayozuia na kudhibiti ugonjwa huo, sababu za ongezeko hilo ni kutokana na kucheleweshwa kwa matokeo ya maabara baada ya watu kufanyiwa vipimo.

Kuna pia ukosefu wa vifaa na uzembe katika utekelezaji wa hatua za usafi. Wakuu wa mkoa wanaeleza kuwa sababu kubwa ya ongezeko hilo ni kutokana na kuwa watu hukusanyika wakati misiba na harusi, na hapo nidipo unakuta watu wanaambukizana virusi hivyo.

Kwa upande wa wakuu wa mkoa huo, uvaaji wa barakoa unatakiwa kuwa wa lazima na ukaguzi unatakiwa kuimarishwa, bila kusahau uwezekano wa kuwasiliana na viongozi wa makanisa, shule na vyombo vya habari.

Hayo yanajiri wakati makanisa yamefunguliwa tena nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, baada ya kufungwa kwa miezi mitano kutokana na janga hilo la Corona.

Siku ya Jumapili, waumini wa Kanisa Katoliki walifurika katika Kanisa kuu la Notre Dame wakiwa wamevalia barakoa kuendelea kujikinga dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo, ambavyo vimewaambukiza watu zaidi ya Elfu Tisa na kusababisha vifo vya watu 240 nchini kote DRC.