DRC-USALAMA

DRC: Kumi na wawili wauawa katika shambulio la watu wenye Mashariki mwa DRC

Vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini DRC kutoka Guatemala na Bengladesh  vikiwa tayari kukabiliana na makundi yenye silaha,katika operesheni iliyoitwa 'UPPERCUT' Machi 14, 2014, huko Bunia, Ituri.
Vikosi vya Umoja wa Mataifa nchini DRC kutoka Guatemala na Bengladesh vikiwa tayari kukabiliana na makundi yenye silaha,katika operesheni iliyoitwa 'UPPERCUT' Machi 14, 2014, huko Bunia, Ituri. Photo MONUSCO / Force

Watu 12 wameuwa hivi punde Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo baada ya kushambuliwa na watu wenye silaha katika mji wa Mwenda mkoani Kivu Kaskazini na Murubia huko Ituri.

Matangazo ya kibiashara

Usalama unaendelea kuzorota katika baadhi ya maeneo ya mikoa ya Kivu Kaskazini na Ituri. Wakaazi wa eneo la Mwenda, Wilayani Beni wamelazimika kuyahama makazi yao, baada ya kuripotiwa visa mbalimbali vya mashambulizi.

“Eneo la Mwenda lilivamia na watu wenye silaha, watu wanane wameuawa na wengine wametekwa nyara, na kwa sasa hatujui waliko. Hali ni ya huzuni hapa kwetu, “ amesema Godefroid Sikumbili, mmoja wa viongozi maeneo ya Mwenda.

Idadi hiyo ya watu wanane, imefanya jumla ya watu 16 kuuawa kikatili katika kipindi cha siku Tatu.

Na katika mkoa wa Ituri hali ya usalama imeendelea kudorora. Akihojiwa na Radio Okapi , Wilson Mugara, mmoja wa madiwani waliochaguliwa katika maeneo ya Murubia amedai kuwa watu 7 wameuawa na Ng'ombe 200 wameibiwa na waasi , taaarifa ambayo bado inachunguzwa, amesema Msemaji jeshi mkoani Ituri, Luteni Jules Ngongo.

"Hadi sasa hatujapata taarifa zaidi kutoka Murubia. Lakini askari wetu wako sehemu hiyo. Na kuhusu shambulizi la jana, liliendesgwa na waasi kutoka eneo linalojulikana kama Chini ya Kilima , wengi wao wakiwa ni kutoka jamii ya Wabira, " amesema Jules Ngongo.

Serkali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo inayashtumu makundi ya ADF na Codeco kuendelea kuhatarisha usalama katika mikoa ya mashariki mwa DRC.