MSUMBIJI-Al SHABAB-SADC-USALAMA

Mkutano wa kilele wa SADC kujadili tishio la kigaidi nchini Msumbiji

Askari wa Msumbiji Machi 7, 2018 huko Mocimboa da Praia, baada ya shambulio la watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa wanajihadi katika mkoa eneo hilo. Mkoa wa Cabo Delgado, unaopakana na Tanzania, umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya wanajihadi tangu Oktoba
Askari wa Msumbiji Machi 7, 2018 huko Mocimboa da Praia, baada ya shambulio la watu wenye silaha wanaoshukiwa kuwa wanajihadi katika mkoa eneo hilo. Mkoa wa Cabo Delgado, unaopakana na Tanzania, umekuwa ukilengwa na mashambulizi ya wanajihadi tangu Oktoba ADRIEN BARBIER / AFP

Viongozi nchi zinazounda Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC, wanakutana katika mkutano wa kilele Jumatatu hii, Agosti 17. Moja ya ajenda katika mkutano huo ni tishio la kigaidi nchini Msumbiji.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano, wanamgambo wa kijihadi walivamia bandari ya Mocimboa da Praia, eneo la kimkakati kwa mradi mkubwa wa gesi asilia (LNG) katika mkoa huo, moja ya uwekezaji mkubwa barani Afrika, ambapo kampuni ya Ufaransa ya Total inashiriki. Shambulio hili limeonyesha wasiwasi kwa nchi za kusini mwa Afrika kuwa zinapaswa kusimamia usalama nchini Msumbiji, la sivyo kuna hatari makundi ya kigaidi yaendelee kuhatarisha usalama katika kanda nzima.

Kwa mujibu wa mwandishi wetu huko Johannesburg, Noé Hochet-Bodin Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC, inasema kuwa ina wasiwasi juu na kundi hili la kijihadi, ambalo limekuwa likiendesha harakati zake kwa miaka 3 kaskazini mwa Msumbiji, karibu na mpaka na Tanzania.

Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika, SADC, inasubiri kuchukuwa hatua ili kulishughulikia kundi hilo tangu tu magaidi walipovamia bandari ya Mocinboa da Praia, eneo la kimkakati kwa kampuni za kimataifa zinazozalisha mafuta ambazo zinatarajia kutoa kiasi kikubwa cha gesi asilia.

Kwa mujibu wa Eric Morier-Genoud, mtafiti kuhusu nchi ya Msumbiji katika Chuo Kikuu cha Belfast, shambulio hili ni ushindi mkubwa kwa kundi la Al shabab, kwa sababu usalama uliimarishwa na vikosi maalum. Siku chache zilizopita, kundi la Al shabab lilitangaza kwamba linajipanga kudhibiti eneo hilo ili kulifanya mji mkuu wao.

Mocimboa da Praia, mji ambako kwa sehemu kubwa wanatoka viongozi wa waasi, pia ni eneo la kimkakati kwa wanajihadi wao, linapatikana kilomita sitini kutoka maeneo ya gesi asilia inayokadiriwa kuwa na thamani ya dola bilioni 60.

Mocimboa da Praia
Mocimboa da Praia Google Maps