DRC-SIASA-USALAMA

DRC: Zaidi ya kumi waangamia katika mapigano ya makundi hasimu yenye silaha Ekengya-Bulembo

Hali ya usalama katika mkoa wa Kivu Kusini inaendelea kutisha kutokana na mapigano ya mara kwa mara na kusababisha wakazi wa maeneo mbalimbali hasa katika wilaya ya Fizi kutoroka makazi yao.
Hali ya usalama katika mkoa wa Kivu Kusini inaendelea kutisha kutokana na mapigano ya mara kwa mara na kusababisha wakazi wa maeneo mbalimbali hasa katika wilaya ya Fizi kutoroka makazi yao. Google Maps

Watu zaidi ya kumi wameuawa wakati wa Mapigano makali kati ya kundi la wapiganaji wa Yakutumba na kikundi cha wapiganaji wenye silaha maarufu Biloze Bishambuke, mwishoni mwa wiki, huko Ekengya-Bulembo, kwenye umbali wa kilomita 16 kusini magharibi mwa wilaya ya Fizi, Kivu Kusini, Mashariki mwa DRC.

Matangazo ya kibiashara

Maafisa wa Usalama katika eneo hilo lenye milima wanasema mapigano hayo yaliyofanyika siku ya jumapili iliyopita yamesababisha mamia ya watu kuyahama makazi.

Umoja wa mataifa nchini DRC MONUSCO umesema kuwa umesikitishwa na mapigano ambayo yamekuwa yakifanyika mara kwa mara.

Mwishoni mwa mwezi Julai watu 12 waliuawa kwa risasi na askari ambao inadaiwa kuwa alikuwa katika hali ya ulevi. Tukio hilo lililotokea katika eneo la Sange, katika mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa DRC.

Hali ya usalama katika mkoa wa Kivu Kusini inaendelea kutisha kutokana na mapigano ya mara kwa mara na kusababisha wakazi wa maeneo mbalimbali hasa katika wilaya ya Fizi kutoroka makazi yao.