MALI-SIASA-USALAMA

Hali ya wasiwasi yatanda nchini Mali baada ya milio ya risasi kusikika katika kambi ya jeshi ya Kati

Wanajeshi wa Mali walioasi katika kambi ya jeshi ya Kati.
Wanajeshi wa Mali walioasi katika kambi ya jeshi ya Kati. Reuters/Luc Gnago

Kambi ya jeshi ya 'Soundiata Keïta' ya Kati bado iko chini ya udhibiti wa kundi la wanajeshi "walioasi". Wanajeshi hao wenye hasira wana silaha mbalimbali za kivita na vifaa mbalimbali vya jeshi ambavyo vinaweza kuhimili mapigano.

Matangazo ya kibiashara

Mashahidi wanasema milio ya risasi inaendelea kusikika karibu na kambi hiyo ya askari walioasi.

Lakini wanajeshi hao wenye hasira hawadhibiti kambi tu, bali pia barabara zinazoelekea katika mji mkuu wa Mali, Bamako.

Wana hasira, wamesema, na hawajatoa maelezo zaidi kufikia sasa. Maafisa wawili ndi wanaongoza kundi hilo la wanajeshi walioasi. Wameagiza kukamatwa maafisa kadhaa waandamizi wa jeshi la Mali. Duru za kuaminika zinabaini kwamba viongozi kadhaa wa kiraia pia wamekamatwa.

Usafiri na shughuli katika maeneo mbalimbali katika mhi wa Bamako, zimestishwa, na milio ya risasi imesikika pia karibu na kambi nyingine ya kikosi cha ulinzi wa taifa.

Wafanyakazi kadhaa wa shirika la utangazaji la ORTM wamelazimika kurejea nyumbani. Katika ofisi zingine za serikali, wafanyakazi wamelazimika "kuondondoka".

Serikali ya Mali bado haijatoa taarifa yoyote kuhusiana na hali hii. Hali ambayo huenda ikabadili taswira saa chache zijazo.