MALI-USALAMA

Mali: Ripoti ya UN yashutumu usalama wa taifa kwa kuzuia mchakato wa amani

Maafisa wa usalama na maafisa waandamizi wa jeshi la Mali wananyooshewa kidole cha lawama katika ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mali.
Maafisa wa usalama na maafisa waandamizi wa jeshi la Mali wananyooshewa kidole cha lawama katika ripoti ya Umoja wa Mataifa kuhusu Mali. AFP/Sebastien Rieussec

Ripoti ya wataalam wa Umoja wa Mataifa kuhusu Mali bado haijawekwa hadharani, lakini tayari imeitilia lawama idara ya usalama wa taifa nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Tofauti na zile zilizotangulia, zilizoyanyooshea kidolea chalawama makundi yenye silaha, ripoti hii inawahusisha moja kwa moja viongozi kwa kuzuia kutekelezwa kwa makubaliano ya amani yaliyofikiwa mwaka 2015.

Wataalam wanainyooshea kidolea cha lawama idara ya Usalama wa taifa na maafisa wake wakuu kadhaa.

Wataalam wa Umoja wa Mataifa wanasema kuwa idara ya usalama wa taifa nchini Mali imekuwa chombo katika huduma ya "mkakati usio rasmi". Mkakati uliyotengenezwa "na kundi dogo la watu walio na ushirikiano wa karibu na rais" kulingana na wataalam hao, na ambao wanalenga kuchelewesha utekelezaji wa mkataba huo.

Ripoti hiyo inabaini kwamba idara ya ujasusi ya Maliilichochea mgawanyiko wa makundi kadhaa yenye silaha, hasa muungano wa CMA. Ili kufikia hatua hiyo, SE - kama inavyoitwa - iliunda kundi muungano mwingine na kuuita jina la CME mnamo mwaka 2017. Mohamed Ousmane Ag Mohamedoune anayeongoza muungano huo mpya, kulingana na ripoti hiyo, ni mmoja wa viongozi wa muungano huo wanaolindwawa na idara ya Usalama wa taifa. Hata hivyo yuko chini ya vikwazo vya Umoja wa Mataifa.

Hayo yanajiri wakati maandamano ya kumtaka rais Ibrahi boubacar Keita ajiuzulu yanaendelea katika maeneo malimbali nchini Mali.