MSUMBIJI-Al SHABAB-SADC-USALAMA

SADC yaunga mkono vita dhidi ya ugaidi Msumbiji

Watu 1,500 wameuwa na wengine zaidi ya Laki Mbili kuyakimbia makwao tangu kuzuka kwa ugaidi mwaka 2017 na wiki iliyopita, magaidi hao walidhibiti bandari ya Mocimboa da Praia.
Watu 1,500 wameuwa na wengine zaidi ya Laki Mbili kuyakimbia makwao tangu kuzuka kwa ugaidi mwaka 2017 na wiki iliyopita, magaidi hao walidhibiti bandari ya Mocimboa da Praia. Lusa

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa bara la Afrika SADC, wamesema wanaunga mkono juhudi za Msumbiji kupambana na ugaidi, baada ya kundi la kijihadi kuteka eneo lenye utajiri wa mafuta Kaskazini mwa nchi hiyo eneo ambalo Kampuni ya Ufaransa Total imewekeza Dolla Bilioni 23.

Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imetolewa na viongozi hao kutoka nchi 16 baada ya kufanya kikao kupitia njia ya mtandao, huku wakiunga mkono jitihada zinazofanywa na Msumbuji kushinda ugaidi.

Hata hivyo, wachambuzi wa mambo wanaona kuwa kauli kutoka kwa wakuu hao wa SADC, haitoshi na hawakuja na mpango madhubuti wa kuisaidia Msumbiji.

Liesl Louw-Vaudran, mtafiti kutoka kituo kinachoshughulikia masuala ya usalama, ISS, nchini Afrika Kusini, ameliambia Shirika la Habari la AFP kuwa, inasikitisha kuwa, baada ya kikao hicho, inaonekana kuwa Msumbiji imeachiwa jukumu la kupambana peke yake.

Jeshi la Msumbiji limetafuta ushauri na usaidizi kutoka jeshi binafsi kutoka nchini Urusi na Afrika Kusini, lakini wachambuzi wa masuala ya usalama wanahisi kuwa hili halitakuwa na matokeo chanya kwa sababu huenda makundi hayo ya kigaidi yakasambaa katika mataifa jirani.

Watu 1,500 wameuwa na wengine zaidi ya Laki Mbili kuyakimbia makwao tangu kuzuka kwa ugaidi mwaka 2017 na wiki iliyopita, magaidi hao walidhibiti bandari ya Mocimboa da Praia.