MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

ECOWAS kujadili mzozo wa Mali

Wanajeshi wa Mali katika kambi ya Kati, Agosti 19, 2020.
Wanajeshi wa Mali katika kambi ya Kati, Agosti 19, 2020. ANNIE RISEMBERG / AFP

Viongozi kutoka Jumuiya ya nchi za Afrika Magharibi ECOWAS wanakutana leo kwa njia ya video, kujadili mapinduzi ya kijeshi yaliyokea nchini Mali na kusababisha rais Ibrahim Boubacar Keita, na serikali yake kujiuzulu.

Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya ECOWAS ambayo imelaani mapinduzi hayo, imekuwa ikisuluhisha mzozo wa kisiasa nchini Mali kabla ya kutokea kuwa mapunduzi hayo ambayo imelaani vikali.

Tayari Kanali Assimi Goita amejitangaza kiongozi wa serikali na kuungwa  mkono na upinzani, huku jeshi likiahidi kuwa madaraka yatakabidhiwa kwa kiongozi wa kiraia, lakini haijafahamika lini.

Katika taarifa iliyotolewa na rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ambaye ni raisa aw Umoja wa Afrika "amelaani kitendo cha kubadili madaraka kinyume na katiba nchini Mali" na "amelitaka jeshi kumuachilia rais IBK, waziri mkuu na mawaziri wengine", na kutoa wito kwa jeshi "kurudi makambini”.

Umoja wa Mataifa, Ufaransa, Umoja wa Ulaya zote zimelaani uasi huo na kuonya juu ya jaribio lolote la kubadili madaraka kinyume na katiba katika taifa hilo. Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametaka "kuachiwa haraka na bila masharti" kwa rais Keita na Waziri Mkuu Cisse.

Kupitia taarifa yao iliyorushwa moja kwa moja na kituo cha televisheni cha taifa baada ay mapinduzi hayo, msemaji wa kundi la wanajeshi walioasi, Kanali Ismael Wague, alisema waliamua kuchukua uamuzi huo ili kuzuia nchi hiyo kutumbukia kwenye machafuko zaidi.

Kanali Ismael Wague aliyakaribisha makundi ya kiraia na vyama vya siasa kujiunga pamoja na kutayarisha muongozo wa kipindi cha mpito utakaowezesha kufanyika Uchaguzi Mkuu.