NIGERIA-USALAMA

Jeshi la Nigeria ladhibiti mji wa Kukawa kutoka mikononi mwa wanajihadi

Wanajeshi wa jeshi la Nigeria wakati wa mazoezi ya kijeshi, Aprili 2018 (Picha kumbukumbu).
Wanajeshi wa jeshi la Nigeria wakati wa mazoezi ya kijeshi, Aprili 2018 (Picha kumbukumbu). STEFAN HEUNIS / AFP

Jeshi la Nigeria limesema limefanikiwa kutwaa miji ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo,ambayo imetawaliwa muda mrefu na wapiganaji wa kijihadi.

Matangazo ya kibiashara

Watu wengi walikuwa wakishikiliwa mateka katika miji hiyo hususan mji wa Kukawa, katika Jimbo la Borno moji hiyo

Msemaji wa wizara ya ulinzi John Eneche amesema baada ya shambulizi la Jumanne lilotibuliwa, jeshi sasa limekita eneo hilo na pana usalama.

“Hakuna mateka tena” , amesema msemaji wa jeshi Meja Jenerali John Eneche.

Siku ya Jumatano, kiongozi wa kundi la wanamgambo wa eneo hilo alionya kwamba kundi la Islamic State katika Afrika Magharibi lilikuwa limewashikilia mateka mamia kadhaa ya watu katika mji wa Kukawa.

Magaidi hao walivamia mji huo Jumanne wiki hii, na kuwashikilia mateka mamia ya raia ambao walikuwa wamerudi majumbani mwao baada ya miaka miwili wakiishi katika kambi za wakimbizi wa ndani. Jiji la Kukawa sasa liko chini ya "udhibiti kamili" wa vikosi vya usalama, ambavyo vimewatia moyo wakaazi wa jiji hilo 'kuanza shughuli zao za kawaida'.

Katika taarifa yake, msemaji wa jeshi la Nigeria amesema kuwa magaidi 8 waliuawa katika mapigano ya kudhibiti mji huo. Kwa upande wake, jeshi limetangaza kupoteza askari wake 3 na wengine 2 kujeruhiwa.