MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mali: ECOWAS yataka IBK kurejeshwa kwenye wadhifa wake

ECOWAS imechukuwa hatua za kuzuia uingiaji wa fedha  na shughuli mbalimbali za kiuchumi pia zimesitishwa, isipokuwa madawa, mafuta na umeme.
ECOWAS imechukuwa hatua za kuzuia uingiaji wa fedha na shughuli mbalimbali za kiuchumi pia zimesitishwa, isipokuwa madawa, mafuta na umeme. Cdéao/Reuters

Viongozi wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wametangaza kutuma haraka ujumbe wake wa ngazi ya juu nchini Mali kwa minajili ya kurejesha taasisi zilizochaguliwa kikatiba, na pia kuchukuwa hatua kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

ECOWAS inaomba Ibrahim Boubacar Keïta na viongozi waachiliwe huru mara moja, na hasa rais IBK arejeshwe kwenye wadhifa wake kama rais wa Mali.

Wakati huo huo, ECOWS imefutilia mbali uhalali wowote wa Kamati kuu ya kitafa (CNSP) iliyoundwa na kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi, na kuomba vikwazo dhidi ya wanajeshi waliofanya mapinduzi hayo pamoja na wasaidizi wao.

"Wakati wa mapinduzi umekwisha," imekumbusha ECOWAS na huu ni ujumbe ambao imekusudia kutolmea kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi. Mali pia imesimamishwa katika taasisi zote za maamuzi za ECOWAS.

Mipaka ya nchi kavu na angani ya Mali imefungwa na nchi za ECOWAS.

ECOWAS imechukuwa hatua za kuzuia uingiaji wa fedha na shughuli mbalimbali za kiuchumi pia zimesitishwa, isipokuwa madawa, mafuta na umeme.

"Nadhani vikwazo hivi [vile vilivyochukuliwa na ECOWAS] ni vikali. Na ninaelewa kabisa kuwa ECOWAS imechukuwa maamuzi kwa misingi wa mikataba na itifaki zake " , amesema Moussa Mara, Waziri Mkuu wa zamani wa Mali.

Wakati huo huo wanajeshi wa Mali waliofanya mapinduzi dhidi ya rais wa nchi hiyo Ibrahim Boubakar Keita wameahidi kuunda serikali ya mpito.