DRC-KAMERHE-HAKI

DRC: Kesi ya Vital Kamerhe yaahirishwa kwa mara ya tatu hadi septemba 18

Vital Kamerhe, mkurugenzi wa zamani kwenye ofisi ya rais wa DR Congo, Félix Tshisekedi.
Vital Kamerhe, mkurugenzi wa zamani kwenye ofisi ya rais wa DR Congo, Félix Tshisekedi. RFI/Sonia Rolley

Kesi ya mkurugenzi wa zamani katika ofisi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Vital Kamerhe, imeahirishwa kwa mara nyingine katika Mahakama ya Rufaa na imepangwa kusikilizwa Septemba 18 mwaka huu.

Matangazo ya kibiashara

Sababu zilizotolewa ni kwamba pande zote katika keshi hiyo hazikupewa taarifa ya tarehe iliyokuwa imepangwa kusikilizwa kwa kesi hiyo.

Hali hii haiwezi kuruhusu jaji kujadili na mawakili kuhusu undani wa kesi hiyo. Muda wa ziada umetolewa ili kumruhusu karani kurekebisha tatizo hilo.

Mawakili wa Vital Kamerhe wanasema wamesikitishwa na uamuzi huo wa mahakama na kubani kwamba "karani hana uwezo wa kurekebisha tatizo liliopo". Wameshauri kwamba karani huyo asaidiwe na mwanasheria mwingine ili kuzuia hali iliyojitokeza kurudi kujitikeza tena.

Kwa upande wake Vital Kamerhe ameendelea kukanusha tuhuma zinazomkabili.

Upande wake wa utetezi umewasilisha tena ombi jipya la kutaka mteja wake aachiliwe kwa dhamana.

Hata hivyo wanasheria hao wana imani kwamba mteja wao sasa ataachiliwa huru. Wamebaini kwamba hali ya afya ya mteja wao inazidi kuwa mbaya.