DRC-KAMERHE-UCHUMI-HAKI

DR Congo: Ombi la Vital Kamerhe kutaka aachiliwe kwa dhamana lakataliwa

Vital Kamerhe, picha iliyopigwa Novemba 11, 2018 huko Geneva.
Vital Kamerhe, picha iliyopigwa Novemba 11, 2018 huko Geneva. Fabrice COFFRINI/AFP

Mahakama ya juu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefutilia mbali ombi la Vital Kamerhe la kutaka kuachiliwa kwa dhamana. Hatua hiyo ya Mahakama ilichukuliwa Jumamosi Agosti 22.

Matangazo ya kibiashara

Vital Kamerhe alihukumiwa kifungo cha miaka 20 katika kesi inayohusiana ujenzi wa makaazi ya polisi na maafisa wa jeshi jijini Kinshasa.

Vital Kamerhe anashtumiwa kutumia vibaya zaidi ya dola milioni 50 za Kimarekani zilizokuwa zimetengwa kugharamia ujenzi wa makaazi ya polisi na maafisa wa jeshi jijini Kinshasa.

Hii ni mara ya tisa ombi lake la kutaka aachiliwe huru kwa dhamana linakataliwa. Mawakili wake wanabaini kwamba hali yake ya afya inazorota na ndi sababu waliomba aweze kuachiliwa kwa dhamana. "Majaji wametangaza kwamba hawakuridhishwa na madai ya ya mawakili wa Vital Kamerhe na kwamba ombi hilo la kuachiliwa huru kwa dhamana halina msingi.

Vital kamerhe Mkurugenzi wa zamani wa ofisi ya rais Felix Tshisekedi bado anasubiri maamuzi ya kesi yake.

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya DRC kuona afisa mwandamizi akihukumiwa na kufungwa jela akiwa anatekeleza majukumu yake serikalini.