MAURITANIA-OUL ABDEL AZIZI-HAKI-UCHUMI

Mauritania: Aliyekuwa rais wa Mauritania Mohamed ould Abdel Aziz aachiliwa huru

Rais wa zamani wa Mauritania (kushoto) ameachiliwa huru. Hapa akiwa nyumbani kwake na wakili wake, wakili Takioullah Eidda.
Rais wa zamani wa Mauritania (kushoto) ameachiliwa huru. Hapa akiwa nyumbani kwake na wakili wake, wakili Takioullah Eidda. RFI

Rais wa zamani wa Mauritania, Mohamed Ould Abdel Aziz, ameruhusiwa kurudi nyumbani usiku wa Jumapili kuamkia Jumatatu 24 Agosti, huku wafuasi wake wakisherehekea kile ambacho wamesema ni ushindi 'mkubwa' kwa kiongozi wao.

Matangazo ya kibiashara

Muda mfupi baada ya saa saba usiku, Mohamed ould Abdel Aziz aliondoka makao makuu ya usalama, ambapo alikuwa anazuiliwa tangu Jumatatu ya wiki iliyopita.

Familia yake na wanasheria wake ambao awali walilani mazingira ya kukamatwa kwake na kuzuiliwa kwake, wamesema kuwa wameridhishwa kurudi kumuona tena huru rais huyo wa zamani.

Wachunguzi walikuwa wanataka kumsikiliza Mohamed ould Abdel Aziz juu ya madai ya matumizi mabaya ya mali ya umma wakati alipokuwa madarakani kwa muongo mmoja. Mashitaka hayo yalitolewa na tume ya bunge ambayo iliwasilisha ripoti yake kwa mahakama mapema mwezi Agosti.

Lakini kwa wiki nzima, aliendelea na msimamo wake wa kusalia kimya.

Hata hivyo yeye na mawakili wake walidai kuwa kukamatwa kwake ni kinyume cha sheria.

"Mohamed ould Abdel Aziz hakutaka kushirikiana na wachunguzi," mmoja wa wanasheria wake. Mteja wetu amesema na ana haki, kuwa alikuwa mbele ya wachunguzi wabaya kwa sababu ana kinga ya kikatiba. Anaweza kuhukumiwa au kuchunguzwa mbele ya Mahakama ya kuu ya Jamhuri ya Kiislamu ya Mauritania, na hapo ni kwa kosa la uhaini mkubwa. Madai ambayo hayahusiani na hilo. Tumefurahi sana na tumeridhishwa na kuachiliwa kwake huru, " wakili Takioullah Eidda, amesema

Hakuna mashitaka yanayomkabili aliyoambiwa Jumapili jioni. Aiombwa tu asiondoke nchini. Mawakili wake wamesema wako tayari kupambana ili haki za mteja wao ziheshimishwe.