DRC-USALAMA

DRC: Makundi ya wanamgambo yasaini mkataba wa kusitisha mapigano

Bunia, mji mkuu wa Ituri.
Bunia, mji mkuu wa Ituri. HokieRNB/CC/Wikimedia Commons

Viongozi wa zamani wa kivita waliotumwa mapema mwezi Julai na rais Felix Tshisekedi katika mkoa wa Ituri kujadili namna ya kusitisha mapigano na wanamgambo wa Codeco wanasema wana matumaini ikilinganishwa na nusu ya matokeo ya kazi yao.

Matangazo ya kibiashara

Lakini mbali na matumani yao, hali inatisha katika mkoa huo. Na mbaya zaidi, wanamgambo hao hawaitii amri kutoka kwa kiongozi wao, kila mmoja anafanya anachokitaka na madai yao hayaeleweki.

Wiki iliyopita, makundi mawili, ambayo wanasema yanawakilisha maelfu ya wapiganaji miongoni mwa wanamgambo hao, yalitia saini kwenye mkataba wa kusitisha mapigano ya upande mmoja. Wanasema wanataka kuonyesha nia yao nzuri tu.

Katika makubaliano yao na ujumbe kutoka Kinshasa, wanamgambo hao walikubaliana kutoshambulia vikosi vya usalama na kurahisishia wafanyakazi wa mashirika ya misaada kufanya shughuli zao.

Makundi hayo mawili ya wanamgambo yanayopiga kambi karibu na eneo la Walendu Pitsi, katika wilaya ya Djugu, pia yamesema yako tayari kushiriki katika mpango wa kuwarejesha katika maisha ya kiraia na wengine kuingizwa katiika idara za usalama na ulinzi.

Lakini kazi bado ni kubwa, hasa katika eneo lenye madini mengi kusini mwa wilaya ya Djugu. Wanamgambo wengine kadhaa wenye silaha ambao wamejikusanya kwa makundi madogo wanapanga sheria, wanafanya wanachokitaka na wanaendelea kutekeleza mauaji dhidi ya raia.

Mpango mwingine wa amani unaoendelea ni ule wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO. Haishiriki katika mchakato huo, unaoendeshwa na viongozi wa zamani wa kivita wanaoshtumiwa kwa makosa makubwa, pia unafanya vikao vya mazungumzo ya kijamii katika mkoa huo.