SUDANI-MAREKANI-USHIRIKIANO

Marekani yaangazia suala la Sudan kuondolewa kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi

Waziri Mkuu, Abdallah Hamdok, wakati wa kuapishwa kwake Khartoum, Agosti 21, 2019.
Waziri Mkuu, Abdallah Hamdok, wakati wa kuapishwa kwake Khartoum, Agosti 21, 2019. Ebrahim HAMID / AFP

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok amesema amekuwa na mazungumzo ya 'moja kwa moja na ya wazi' huko Khartoum Jumanne wiki hii na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Mike Pompeo, wakijadili hasa suala la Sudan kuondolewa kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi.

Matangazo ya kibiashara

Waziri huyo wa mambo ya nje wa Marekani amewasili nchini Sudani kwa ndege ya moja kwa moja kutoka Tel Aviv kwenda Khartoum, ikiwa ni ziara ya kwanza ya kiongozi wa juu nchini Marekani kuzuru nchi hiyo katika kipindi hiki nchi nyingi zikipambana dhidi ya ugonjwa wa Corona.

Marekani inajaribu kuendeleza uhusiano wa karibu kati ya nchi hiyo ya Afrika na Israeli.

Ziara ya Mike Pompeo nchini Sudan ni sehemu ya ziara ya kikanda ya waziri wa Marekani mwenye dhamana ya Mambo ya Nje kujaribu kuonyesha ubora na umuhimu nchi zingine za Kiarabu mkataba kati ya Umoja aw Falme za Kiarabu na Israeli uliyofikiwa mapema mwezi huu, ambao unaolenga kufufua kikamilifu uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Uhusiano na Israeli ni suala nyeti nchini Sudani, nchi ya Kiislamu ambayo ilikuwa moja ya maadui wakuu wa Israeli wakati wa utawala wa Omar al-Bashir, aliyetimuliwa madarakani na jeshi mwezi Aprili 2019.

Uhusiano wa Sudan na Marekani pia umeendelea kukumbwa na sintofahamu kwa sababu ya vikwazo vilivyowekwa na utawala wa Marekani, vinavyohusiana na madai ya Khartoum kusaidia makundi yenye silaha na vita vya wenyewe kwa wenyewe huko Darfur.

Ingawa vikwazo vyabiashara vimeondolewa tangu mwaka 2017, Sudan bado iko kwenye orodha ya Marekani ya nchi zinazounga mkono ugaidi, hali inayozuia nchi hiyo kupata ufadhili wa kimataifa.