MALI-OIF-SIASA-USHIRIKIANO

Mali yasimamishwa kwenye uanachama wa OIF

Ujumbe wa ECOWAS ukikutana kwa mazungumzo na viongozi kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi Mali, huko Bamako, Agosti 22.
Ujumbe wa ECOWAS ukikutana kwa mazungumzo na viongozi kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi Mali, huko Bamako, Agosti 22. REUTERS/Mamadou Keita

Jumuiya ya kimataifa ya Francophonie imechukua uamuzi baada ya Jumuiya ya Mataifa ya Afrika Magharibi, ECOWS, wa kusimamisha nchi ya Mali kwenye uanachama wa jumuiya hiyo, siku chache baada ya jeshi kufanya mapinduzi dhidi ya utawala wa Ibrahim Boubacara Keita.

Matangazo ya kibiashara

OIF imebaini kwamba hatua zote za ushirikiano ambazo zinafaidi raia zitaendelea. Vile vile na zile zinazoweza kukuza au kuendeleza demokrasia nchini Mali. Baraza la Kudumu la Francophonie limelitaka jeshi kutoa haraka muda unaowezekana kwa kuunda serkali ya mpito itakayoongozwa kiraia.

Kundi la wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali tangu walipompindua madarakani rais Ibrahim Boubacar Keita Agosti 18, wanataka kuundwa kwa serikali ya mpito ambayo itaongozwa na mwanajeshi kwa kipindi cha miaka mitatu.

Hivi karibuni ujume wa jeshi na ECOWAS walikutana, lakini walishindwa kufikia mwafaka kuhusu uhamishaji wa madaraka

Ujumbe wa upatanishi kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Mahgaribi (ECOWAS) na baraza la kijeshi la Mali zilishindwa kufikia maafikiano kuhusu suala la kuhamisha madaraka nchini humo.

Msemaji wa Baraza la Taifa la Uokozi wa Watu (CNSP) nchini Mali Kanali-Meja Ismael Wague alisema, hakuna kilichoamuliwa kuhusu suala hilo, muda wa mpito, mwelekeo na uundaji wa serikali itakayowekwa madarakani.

Alisema mfumo wa serikali ya mpito utaamuliwa na wananchi wa Mali wenyewe, na kuongeza kuwa wanawasiliana na ECOWAS na hakuna uamuzi wowote utakaochukuliwa bila ya vyama vya siasa na taasisi muhimu za nchi hiyo kuhusishwa.