MALI-EU-USALAMA-SIASA

Umoja wa Ulaya wasitisha kwa muda ujumbe wake nchini Mali

Mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya, Josep Borrell (picha ya kumbukumbu)
Mkuu wa sera za nje za Umoja wa Ulaya, Josep Borrell (picha ya kumbukumbu) Francisco Seco/Pool via REUTERS

Hali nchini Mali ni miongoni mwa msauala nyeti yaliyojadiliwa na mawaziri wa ulinzi wa nchi za Umoja wa Ulaya wanaokutana tangu jana huko Berlin, nchini Ujerumani.

Matangazo ya kibiashara

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Waziri wa Ujerumani, Annegret Kramp-Karrenbauer, mkuu wa sera za mambo ya nje wa Umoja wa Ulaya Josep Borrell amelaani jaribio la mapinduzi nchini Mali na kuomba kuanzishwa kwa mchakato wa kidemokrasia nchini humo.

"Ujumbe wetu nchini Mali umesimamishwa kwa muda lakini utaanza tena haraka iwezekanavyo. Umoja wa Ulaya imewekeza sana nchini Mali na hatutaki kuona juhudi zilizofanywa zikipotea, " amesema Josep Borrell.

Umoja wa Ulaya unatoa mafunzo kwa jeshi la Mali na vikosi vya usalama vya kiraia ili kuimarisha uwezo wake na kuboresha hali ya usalama wa nchi.

Hatua hiyo ya Umoja wa Ulaya inakuja baada ya Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Magharibi, ECOWAS, na Jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa kuchukua hatua kama hiyo.