CONGO-LISSOUBA-SIASA

Familia ya Pascal Lissouba yataka mwili wa marehemu kusafirishwa nchini Kongo-Brazzaville

Pascal Lissouba, rais wa zamani wa Congo-Brazzaville.
Pascal Lissouba, rais wa zamani wa Congo-Brazzaville. AFP/Jamal A. Wilson

Mazishi ya Pascal Lissouba, rais wa zamani wa Congo kati ya mwaka wa 1992 na 1997 ytafanyika Jumatatu wiki ijayo, Agosti 31, huko Perpignan, nchini Ufaransa, ambapo Pascal Lissouba alikuwa anaishi kwa miaka kadhaa na ambapo kifo chake kilitokea Jumatatu, Agosti 23.

Matangazo ya kibiashara

Lakini haya ni mazishi ya muda tu. Familia ya Lissouba inataka mwili wa rais wa zamani uzikwe kwa heshima nchini Congo, katika nchi yake ya asili. Lakini sio kwa sasa, kutokana na mgogoro wa afya unaosababishwa na virusi vya Corona.

Pascal Lissouba atazikwa huko Perpignan, nchini Ufaransa, Jumatatu, Agosti 31 saa 2:30 mchana. Lakini hayo ni mazishi ya muda, limebaini tangazo lililotumwa na familia ya marehemu.

Kwa taarifa, familia ya Lissouba inabainisha kuwa mwili wa rais huyo wa zamani utarudishwa nchini Congo wakati "masharti yote yatakapofikiwa kwa mazishi ya heshima mbele ya familia yake".

Kwa sababu ya hali ya dharura ya kiafya inayohusiana na janga la Corona, haiwezekani kuandaa mkusanyiko wa watu wengi, kwa kupokea mwili wa marehemu, mmoja wa ndugu zake amesema.