MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mali: ECOWAS kutoa ridhaa kuundwa kwa serikali ya mpito kwa mwaka mmoja

Ujumbe wa ECOWAS, ukiongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, ulikutana na kundi la wanajeshi wanaoshikilia madaraka Mali Agosti 22.
Ujumbe wa ECOWAS, ukiongozwa na rais wa zamani wa Nigeria Goodluck Jonathan, ulikutana na kundi la wanajeshi wanaoshikilia madaraka Mali Agosti 22. ANNIE RISEMBERG / AFP

Mkutano wa pili wa wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, unafanyika leo Ijumaa tangu kufanyika kwa mapinduzi nchini Mali.

Matangazo ya kibiashara

Tangu wiki iliyopita kundi la jeshi linaloshikilia madaraka limeendelea kupata shinikizo ili kurejesha taasisi za kiraia zilizochaguliwa.

Wiki iliyopita Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS ililita jeshi kumrejesha madarakani Ibrahim Boubacara Keita, na kuchukua uamuzi wa kufunga mipaka ya nchi wanachama jirani na Mali na kuiwekea nchi hiyo vikwazo vya kiuchumi. Lakini tangu wakati huo jeshi lilianza kulegeza msimamo wake. Jeshi lilikubali kumuachilia huru rais aliyepinduliwa Ibrahim Boubacar Keita.

Wakati huo huo mazungumzo kati ya wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali na ECOWAS kuhusu uundwaji wa serikali ya mpitoa yameanza. Jumuiya hiyo imelitaka jeshi kuunda serikali ya mpito itakayoongoza nchi kwa mwaka mmoja.

ECOWAS "inakubali" wazo la "serikali ya mpito itakayoyoongozwa na raia au mwanajeshi mstaafu" kwa kipindi cha mpito cha "miezi sita, tisa, au kumi na mbili" nchini Mali, kabla ya kufanyika kwa uchaguzi nchini humo, imesema taarifa kutoka ikulu ya rais wa Nigeria. Ikimaanisha kipindi cha mwaka mmoja, wakati jeshi linataka "kukaa madarakani" kwa "miaka mitatu" kabla ya kufanyika uchaguzi, ameripoti mwandishi wetu huko Lagos, Liza Fabbian.