MAURITANIA-OUL ABDEL AZIZI-HAKI-UCHUMI

Abdel Aziz: Kinachonisibu ni siasa

Mohamed Ould Abdel Aziz, rais wa zamani wa Mauritania (picha ya zamani).
Mohamed Ould Abdel Aziz, rais wa zamani wa Mauritania (picha ya zamani). AFP PHOTO / WATT ABELJELIL

Rais wa zamani wa Mauritania Mohamed Ould Abdel Aziz, katika mkutano na waandishi wa habari huko Nouakchott, amelaani kile alichokiita kampeni ya kuchafua jina lake na familia yake.

Matangazo ya kibiashara

Amedai kuwa analengwa na maadui zake kutoka chama tawala na upinzani ambao wanataka kulipiza kisasi kisiasa. Lakini ameahidi kupambana hadi dakika ya mwisho kuonyesha kuwa hana hatia yoyote.

Rais wa zamani wa Mauritania ambaye amlikuwa akihojiwa kwa wiki moja kwenye makao mkauu ya usalama wa taifa kati ya Agosti 17 na 24, amesema "analengwa na maadui zake kisiasa ambao wanataka kujilipiza kisasi' kwa kutaka kuendelea kuwa na udhibiti kwenye chama tawala baada ya kuondoka kwake.

Mohamed Ould Abdel Aziz, akizungumzia juu ya maadui zake, analenga hasa tume ya uchunguzi ya bunge. Wajumbe wake "hawana uwezo wa kufanya kazi yenye uaminifu na ya uwazi," amesema jenerali mstaafu ambaye aliongoza Mauritania kati ya mwaka 2008 na 2019.

Tume ya uchunguzi ya bunge ilitoa ripoti inayonyooshea kidole kashfa ya rushwa na matumizi mabaya ya fedha za umma wakati wa muongo mmoja wa utawala wake.

Rais wa zamani amekanusha matokeo ya ripoti hiyo akibaini kwamba , tume ya uchunguzi ya bunge iliundwa ili kumpaka tope yeye na familia yake. Akizungumzia kuhusu hatma yake, Aziz amesema nia yake ya kuendelea na siasa.