CAR-USALAMA-SIASA

CAR: Catherine Samba-Panza atangaza kuwania katika uchaguzi wa urais

Rais wa zamani wa mpito Catherine Samba-Panza ametangaza nia yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais, Ijumaa Agosti 28 (picha ya kumbukumbu.
Rais wa zamani wa mpito Catherine Samba-Panza ametangaza nia yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais, Ijumaa Agosti 28 (picha ya kumbukumbu. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO

Uchaguzi wa urais nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati umepangwa kufanyika mwezi Desemba mwaka huu. Rais wa zamani wa mpito Catherine Samba-Panza, ambaye hana uhusiano wowote na chama chochote cha siasa, ametangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi huo.

Matangazo ya kibiashara

"Natangaza rasmi kwamba nitawania katika uchaguzi wa urais", ametangaza Catherine Samba-Panza wakati wa hafla huko Bangui, mji mkuu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, iliyoandaliwa na kamati za msaada, akibaini kwamba tayari "aliongoza nchi hii katika mazingira magumu".

Catherine Samba-Panza aliteuliwa kuwa rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati mwezi Januari 2014, ilipokuwa katika vita vya wenyewe kwa wenyewe. Catherine Samba-Panza, ambaye ni mwanamke wa kwanza kushika madaraka katika nchi hii ya Afrika ya Kati, alitoa nafasi kwa Faustin-Archange Touadéra, mshindi wa uchaguzi wa mwezi Machi 2016 na ambaye anapewa na fasi ya kuwania katika uchaguzi huo kwa muhula wa pili mwezi Desemba.

Hata kama chama tawala bado hakijatangaza mgombea, kuna shaka kidogo juu ya nani atapeperusha bendera ya chama cha MCU. Rais anayemaliza muda wake Faustin-Archange Touadéra alitarajiwa kupitishwa wiki hii katika Mkutano Mkuu wa chama tawala, lakini mkutano huo umesogezwa mbele mwezi mmoja. Sababu ya kuahirishwa kwa mkutano huo ni kutopatikana kwa Simplice Mathieu Sarandji, katibu mkuu wa chama, kwa sababu za kiafya.