COTE D'IVOIRE-SORO-SIASA

Cote d'Ivoire: Mahakama yathibitisha kufutwa kwa Guillaume Soro kwenye orodha ya wagombea urais

Kiongozi wa zamani wa waasi na Waziri Mkuu wa zamani Guillaume Soro, kwenye mkutano na waandishi wa habari, Januari 28, 2020 huko Paris. (picha ya kumbukumbu)
Kiongozi wa zamani wa waasi na Waziri Mkuu wa zamani Guillaume Soro, kwenye mkutano na waandishi wa habari, Januari 28, 2020 huko Paris. (picha ya kumbukumbu) Lionel BONAVENTURE / AFP

Mahakama nchini Cote d'Ivoire imethibitisha uamuzi wa Tume huru ya uchaguzi nchini humo kuwa Spika wa zamani wa bunge, Guillaume Soro, hana nafasi ya kuwania katika uchaguzi wa urais ujao nchini Cote d'Ivoire.

Matangazo ya kibiashara

Agosti 18, Tume Huru ya Uchaguzi nchini Cote d'Ivoire ilitoa uamuzi wake katika mzozo juu ya orodha ya wagombea urais. Laurent Gbagbo na Guillaume Soro, walifutwa kwenye orodha hiyo, na baadae walikataa rufaa, lakini uamuzi wa Mahakama ya Abidhjan umekuja kuthibitisha hatua iliyochukuliwa na Tume ya Uchaguzi.

Ferkessédougou, mji ambao Guillaume Soro kawaida alijiandikisha kwenye orodha ya wagombea urais, hauna mahakama. Ililazimika kesi hiyo ipelekwe katika mahakama ya Korhogo, kilomita kadhaa na mji wa Ferkessédougou. Baada ya siku kadhaa za kusubiri, hatimaye uamuzi ulitolewa jana Ijumaa na kubaini kwamba Guillaume Soro hana nafasi ya kuwania kwenye uchaguzi huo.

Kama Laurent Gbagbo, Guillaume Soro amekamilisha vitendo vyake vyote na kwa hivyo amezuiwa kuwania katika uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba, na hata kupiga kura.

Katika agizo lake la Agosti 28, mahakama imeamua kwamba rufaa ya Guillaume Soro haina msingi na halikubaliki, kwani spika wa zamani wa bunge alipoteza haki yake ya kiraia kufuatia hukumu ya kifungo cha miaka 200 dhidi yake kutokana na matumizi mabaya ya fedha za umma.