DRC-USALAMA-SIASA

DRC: Vijana 23 wanaoshukiwa kuunda kundi la wanamgambo wakamatwa Kinshasa

Barabara kuu huko Kinshasa, Agosti 16, 2019.
Barabara kuu huko Kinshasa, Agosti 16, 2019. Photo by Ute Grabowsky/Photothek via Getty Images

Operesheni ya polisi ilifanyika Alhamisi katikati mwa Kinshasa, huko Kingabwa nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Watu ishirini na tatu walikamatwa.

Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa, polisi imesema watu hao waliunda kundi la wanamgambo.

Kundi ambalo, kulingana na watu waliokamatwa, lilitarajia kuchukua nafasi ya polisi na kusimamia usalama kwa kusaidia utawala wa Felix Tshisekedi endapo kutakuwa na jaribio la kuhatarisha usalama.

Polisi hivi sasa imetangaza kukamatwa kwa watu ishirini na tatu. Wengine wamekimbia na wanatafutwa.

Kwa upande wa Marcellin Chisambo, mshauri wa zamani wa kisiasa wa Joseph Kabila, amesema rais Félix Tshisekedi alikuwa na taarifa juu ya uundwaji wa kundi hilo la wanamgambo lililopewa mafunzo huko Kingabwa na baadhi ya askari wa kikosi cha ulinzi wa rais. Jenerali Sylvano Kasongo, mkuu wa polisi katika mji mkuu Kinshasa, amemkataa, kwa sasa, kutoa maoni yoyote juu ya jambo hili.

Naye katibu mkuu wa chama cha rais, Augustin Kabuya, amehoji wale wanaoshutumu chama cha UDPS ikiwa hawana matatizo ya kisaikolojia. amesema, "wanatushtumu mambo ya upuuzi", "wale wanaotufikiria kwa njia hii, nafasi yao ni katika kituo cha wagonjwa wa akili cha CNPP".

Augustin Kabuya ameelezea masikitiko yake akisema, "hatujawahi kufikiria juu ya suala la kuunda kundi la watu wenye silaha wakati tulikuwa katika upinzani, kwa nini tufanya kwa leo wakati tuko madarakani? Hadi lini dhambi zote za Israeli zitabebeshwa chama cha UDPS? », ameongeza katibu mkuu wa chama cha rais, ambaye amebaini kwamba taarifa ya polisi iko wazi. taarifa hiyo hakihusishi chama cha UDPS katika jarubio lolote la kuyumbisha usalama wa nchi.