MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Mali: ECOWAS yasisitiza juu ya kurudi madarakani kwa serikali ya kiraia kwa kipindi cha mpito

Picha ya skrini ya mkutano wa marais wa ECOWAS kupitia video kuhusu Mali, Agosti 20, 2020 (picha ya kumbukubu).
Picha ya skrini ya mkutano wa marais wa ECOWAS kupitia video kuhusu Mali, Agosti 20, 2020 (picha ya kumbukubu). Reuters/Cédéao

Wakuu wa mataifa ya Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) wameutaka uongozi wa kijeshi nchini Mali kwamba hawakubaliani na hoja yao kutaka kutaka kusalia madarakani kwa miaka mitatu kabla ya kukabidhi madaraka kwa raia.

Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao walikutana Ijumaa, Agosti 28 kupitia kujadili hali ya Mali. Hata hivyo viongozi hao hawajathibitisha pendekezo la uongozi wa kijeshi unaoshikilia madarakani nchini Mali, lakini wamepongeza uamuzi waliochukuwa wa kuwaachilia huru viongozi waliokuwa wakiwashikilia, ikiwa ni pamoja na aliyekuwa rais wa nchi hiyo Ibrahim Boubacar Keita (IBK).

Wakati huo huo kundi la wanajeshi lililofanya mapinduzi limeomba miaka miwili au mitatu kuongoza nchi ya Mali kama kipindi cha mpito kukamilisha kipindi cha miaka mitano cha rais aliyetimuliwa madarakani. Uongozi wa kijeshi unataka kuongoza kipindi cha mpito baada ya kuundwa serikali itakayoundwa na raia na wanajeshi.

Wanajeshi hao wamependekeza uchaguzi mwingine ufanyike 2023, jambo ambalo limekataliwa vikali na matiafa 15 yalio katika Jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika Magharibi ECOWAS.

Jean-Claude Kassi Brou, rais wa Tume ya ECOWAS, ameiambia RFI: "Kuna sheria ndani ya taasisi ECOWAS ambayo inasisitiza: kipindi cha mpito kama kutatokea mapinduzi ya kijeshi katika nchi mojawapo ya jumuiya hiii na kipindi hicho hakipaswi kuzidi miezi kumi na mbili" . Ameongeza kuwa: "Sheria nyingine inabaini kwamba rais wa mpito anatakiwa awe raia, sawa na waziri mkuu, lakini asiwe kwenye orodha ya wagombea urais.

Hata hivyo ECOWAS imebaini kwamba vikwazo bado vinatekelezwa na mipaka bado inafungwa. Lakini vikwazo hivyo vinaweza kuondolewa hatua kwa hatua, taarifa ya mwisho ya ECOWAS imeongeza.

Mmoja wa washiriki wa mkutano huo, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, amelitaka jeshi kutii wito wa ECOWAS.

ECOWAS imetoa pendekezo la kuundwa kwa jeshi la dharura, kwa lengo la kwenda kufanikisha utawala wa kiraia, wazo ambalo hata hivyo linaonekana kupignwa kutokana na raia wa taifa hilo kufanya maandamano na kuunga mkono kuondolewa rais wao waliemchagua kidemokrasia.