DRC-ALBINO-MICHEZO

DRC: Bingwa wa zamani wa mieleka Mwimba Texas afariki dunia

Bingwa wa zamani wa mieleka DRC, Mwimba Texas.
Bingwa wa zamani wa mieleka DRC, Mwimba Texas. FMM

Bingwa wa mieleka nchini Jamùhurti ya Kidemokrasia ya Congo, Mwimba Texas, amefariki dunia tangu Jumapili Agosti 30 akiwa na umri wa miaka 53 huko Kinshasa.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na familia yake, alikuwa anaugua kwa siku kadhaa. Kwa mashindano zaidi ya 650, alikuza mieleka ya kitaalam, na kuwaacha watu wengi, hasa nchini DRC wakipigwa na bumbuwazi.

Bingwa wa kwanza wa mieleka kutoka jamii ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Mwimba Texas pia alipambana katika vita dhidi ya ubaguzi unaowakabili watu walio na ulemavu huu wa ngozi.

Mwimba Texas hakushindwa katika mashindano 652, na alikuwa nguli katika mieleka nchini DRC, lakini pia alikuwa maarufu sana nchini DRC kwa kujitolea kwake katika mapambano dhidi ya ubaguzi unaowakabili Maalbino.

Mwaka 1998 bingwa huyo wa zamani wa mieleka pia alizindua shirika lililopewa jina lake, kusaidia wale aliowaita "ndugu zake Maalbino".

Aliwahimiza watu walio ulemavu wa ngozi unaosababishwa na upungufu wa melanini ili kujikinga na jua kwa kuzuia saratani ya ngozi.

Umaarufu wa Mwimba Texas pia umechangia kuongeza uelewa katika jamii ya DRC juu ya hatima ya Maalbino ambao wanauliwa mara kwa mara barani Afrika kwa sababu wanatuhumiwa kuwa ni mashetani na mambo yao menggi yanahusiana na ushirikina.