SUDANI-USALAMA-SIASA

Ipi hatima ya Sudan

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok wakati wa ziara yake jijini Darfur Novemba 4, 2019.
Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok wakati wa ziara yake jijini Darfur Novemba 4, 2019. ASHRAF SHAZLY / AFP

Mkataba wa amani umetiwa sahihi tangu mwishoni mwa Juma hili lililopita na wawakilishi wa serikali ya Sudan na wale wa makundi makuu yenye silaha nchini humo - hasa kutoka Darfur.

Matangazo ya kibiashara

Mkataba huo unalenga kumaliza miaka kumi na saba ya vita vya wenyewe kwa wenyewe. Mkataba huo unatarajiwa kutiwa rasmi saini Jumatatu hii, Agosti 31 huko Juba, mji mkuu wa Sudan Kusini ambapo mazungumzo yalifanyika katika miezi ya hivi karibuni.

Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok aliwasili katika mji wa Juba Jumapili, Agosti 30, alasiri kwa zoezi hili la kutia saini mkataba huo wa kihistoria.

Baada ya mazungumzo ya miezi kumi, Khartoum na makundi makuu yenye silaha huko Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile hatimaye wamekubaliana kuhusu kugawana madaraka, kuhusu usalama, haki, kurudi kwa wakimbizi.

Makundi kadhaa yenye silaha yalitia sahihi kwenye mkataba huo na yako tayari kusaini mkataba wa mwisho leo Jumatatu huko Juba.

Muungano wa makundi yanayotetea mapinduzi nchini Sudan, ambao unajumuisha makundi manne yenye silaha ni miongoni mwa makundi ambayo yako tayari kusaini mkataba huowa kihistoria nchini Sudan.

Kwa mujibu wa msemaji wa muungano huo Mohammed Zakaria, mkataba huu ambao unatarajia kumaliza miaka kumi na saba ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ni ushindi mkubwa.

"Siku chache zilizopita wakati tulitia saini makubaliano juu ya maswala ya usalama - ambayo ni masuala tete zaidi ya mkataba huyu kamili - baadhi ya watu walianza kulia. Iilifurahisa, kwa sababu ni ushindi wa kweli, hasa kwa waathiriwa wote wa mzozo huu. Vurugu hazijaanza mwaka 1989 baada yaOmar al-Bashir kuchukuwa madaraka, ubaguzi, ukosefu wa kugawana madaraka, kugawana rasilimali, vyote vilianza mwaka 1956, baada tu ya uhuru. Na baada ya wakati huu wote, hatimaye tumeweza kupata suluhisho la mgogoro huu, ni ushindi wa kweli. Watu wanaofurahi, sio tu wanasiasa, au makundi yenye silaha, lakini pia vyama vya kiraia, wale wote ambao wanaishi katika kambi za Darfur na ambao wana historia mbaya, ”amebaini Mohammed Zakaria.