CONGO-MOKOKO-SIASA

Jean-Marie Michel Mokoko arejea Brazzaville

Kiongozi wa upinzani Congo, Jean-Marie Michel Mokoko, Machi 19, 2016.
Kiongozi wa upinzani Congo, Jean-Marie Michel Mokoko, Machi 19, 2016. EDUARDO SOTERAS / AFP

Kiongozi wa upinzani nchini Congo Jean-Marie Michel Mokoko, 73, yuko nchini tangu Jumapili Agosti 30. alirejea nchini akitokea nchini Uturuki ambapo alikuwa akipewa matibabu kwa mwezi mmoja uliopita.

Matangazo ya kibiashara

Madaktari wake wanasema anaendelea vizuri. Mashirika ya kiraia zimekaribisha hatua yake ya kurejea nchini na kuomba uangalifu zaidi kwa usalma wake, wakati mamlaka imepongeza hatua ya Jenerali Mokoko na familia yake kwa kuwajibika.

Wakili wake Yvon Ibouanga amesema Jenerali Mokoko amepelekwa katika hospitali ya kijeshi mjini Brazzaville ambako alifanikiwa kwa uchunguzi zaidi wa afya yake. Amesema kiongozi huyo yupo katika hali nzuri.

"Tunatarajia katika siku chache zijazo kuanza utaratibu wa kuomba achiliwa huru," wakili wake mwingine amesema.

Kulingana na chanzo kutoka idara ya magereza, mkuu wa zamani wa jeshi atalazimika atarudishwa katika chumba chake gerezani baada ya kufanyiwa uchunguzi na madaktari.

Jenerali Mokoko aliyepambana na rais mwenye msimamo mkali Denis Sassou Nguesso katika uchaguzi wa 2016, alifungwa miaka 20 jela mwaka wa 2019 kwa mashitaka ya kuhujumu usalama wa taifa na kumiliki silaha kinyume cha sheria.