MALI-SIASA-USALAMA

Mali: Jeshi lafanya uteuzi kwenye nafasi mbalimbali, IBK alazwa hospitalini

Kanali Ismael Wague, msemaji wa Kamati ya Kitaifa ya Wokovu wa wananchi, Bamako  Agosti 24, 2020 (picha ya kumbukumbu)
Kanali Ismael Wague, msemaji wa Kamati ya Kitaifa ya Wokovu wa wananchi, Bamako Agosti 24, 2020 (picha ya kumbukumbu) REUTERS/Moussa Kalapo

Kamati ya Kitaifa ya Wokovu wa Wananchi (CNSP), chombo kilichoundwa na kundi la jeshi lililofanya mapinduzi nchini Mali, Agosti 18, kinaendelea kujidhatiti. Viongozi kadhaa wameteuliwa kwenye nyadhifa mbalimbali wakati rais aliye kuwa Ibrahim Boubacar Keïta akilazwa hospitalini.

Matangazo ya kibiashara

Cheick Oumar Traoré ameteuliwa kuwa mshauri maalum wa kiongozi wa mapinduzi, anayehusika na habari na mawasiliano.

Daktari Youssouf Coulibaly, ni raia mwingine aliyeteuliwa, kwenye nafasi ya mshauri maalum wa kiongozi wa mapinduzi, anayehusika na maswala ya kisheria.

Kwa upande wa jeshi, Jenerali Souleymane Doucouré, kiongozi wa zamani wa msemaji wa sasa wa kundi la jeshi lililofanya mapinduzi wa ameteuliwa kuwa katibu mkuu wa wizara ya ulinzi. Jenerali Oumar Diarra ameteuliwa kuwa Mkuu mpya wa jeshi la Mali. Kundi hilo la wanajeshi waliofanya mapinduzi pia lilifanya mabadiliko mengine kwenye nafasi muhimu jeshini na kwenye idara ya ujasusi.

Wakati huo huo aliye kuwa rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita (IBK) amelazwa hospitalini tangu Jumanne wiki hii katika hospitali moja mjini Bamako. Duru kutoka familia yake zimebaini kwamba anaweza kuruhusiwa kuondoka hospitali leo jioni.

Hata hivyo mmoja kati ya wasaidizi wake amesema kuwa Bw. Keita amekwenda kufanya vipimo vya kawaida vya afya yake hospitali.

Mwanasiasa huyo wa miaka 75 alizuiliwa kwa siku kumi na wanajeshi kabla atangaze kujiuzulu na baaadae kuachiliwa huru.

Wakati wa mazungumzo ya kutafuta mwafaka wa mzozo wa kisiasa nchini Mali Bwana Keita alinukuliwa akisema kuwa hana haja ya mamlaka ya urais.

Kwa miezi kadhaa upinzani ulikuwa ukimshinikiza kujiuzulu na kumlaumu kwa kurudisha nyuma uchumi wa nchi, kudhibiti ufisadi na kushindwa kukabiliana na makundi ya kijihadi.