MALI-BARKHANE-USALAMA

Mali: Mtu mmoja auawa na askari wa kikosi cha Barkhane

Helikopta ya kikosi cha jeshi la Ufaransa cha Barkhane huko Gao (picha ya kumbukumbu).
Helikopta ya kikosi cha jeshi la Ufaransa cha Barkhane huko Gao (picha ya kumbukumbu). AFP Photos/Michele Cattani

Wengi wanajiuliza maswali kuhusu kifo cha mtu mmoja aliyeuawa na askari wa kikosi cha jeshi la Ufaransa nchini Mali, katika tukio lililohusisha basi, karibu kilomita hamsini kutoka Gao.

Matangazo ya kibiashara

Makao makuu ya jeshi la Ufaransa yanasema gari hilo lilikuwa likitembea kwa kasi likielekea kwenye msafara wa jeshi na risasi za tahadhari zilipigwa. Madai yaliyofutiliwa mbali na shirika la uchukuzi ambalo linamiliki basi hilo.

Basi hilo lilikuwa limeabiri watu 45. Lilikuwa likitokea Bamako kuelekea eneo la Gao.

Kulingana na toleo la jeshi la Ufaransa, basi hilo lilikuwa likienda kwa kasi kubwa kuelekea msafara wa jeshi. Wito wa maneno, ishara, risasi la kwanza la onyo, lakini basi hilo halijasimama, kikosi cha Barkhane kimebaini.

Katika eneo hilo, tishio la magari yanayotegwa mabomu ni kubwa. Kikosi cha Ufaransa kinakiri kuwa kulipigwa risasi la pili la onyo lililoelekezwa ardhini.

"Basi lilikuwa likisafiri kwa mwendo wa kilomita 40 kwa saa"

Abdoulaye Haidara, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la uchukuzi la Nour, ambalo linamiliki basi hilo, ametoa toleo lingine kuhusu tukio hilo. “Hakukuwa na risasi za onyo. Basi lilikuwa likisafiri kwa mwendo wa kilomita 40 kwa saa, katika eneo lililo wazi. Basi lilikuwa mita 200 na msafara wa magari ya kikosi cha jeshi la Barkhane."

Kwa vyovyote vile, risasi mbili zilizopigwa inaonekana zilipita kwenye kioo cha mbele cha basi na kujeruhi watu watatu, mmoja wao vibaya. Mtu huyo alifariki dunia muda mfupi baadaye alipokuwa akisafirishwa kwenda hospitalini huko Gao.

Kulingana na jeshi la Ufaransa, hatua zote zimechukuliwa ili kujuwa mazingira ya tukio hilo kwa ushirikiano na polisi ya Mali.