COTE D'IVOIRE-SIASA-USALAMA

Côte d’Ivoire: Upinzani waendelea kupinga hatua ya Ouattara kuwania katika uchaguzi wa urais

Pascal Affi N'Guessan na wengine wanamuomba rais wa Ufaransa kusema ikiwa anaunga mkono au la hatua ya Alassane Ouattara katika uchaguzi ujao wa rais.
Pascal Affi N'Guessan na wengine wanamuomba rais wa Ufaransa kusema ikiwa anaunga mkono au la hatua ya Alassane Ouattara katika uchaguzi ujao wa rais. SIA KAMBOU / AFP

Upinzani nchini Côte d’Ivoire umemuomba rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kuonyesha msimamo wake kuhusu hatua ya rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara kutaka kuwania katika uchaguzi wa urais.

Matangazo ya kibiashara

Wakati rais Alassane Ouattara yuko Ufaransa na anatarajia kukutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mwishoni mwa wiki hii, wanasiasa kadhaa wa upinzani wametoa wito kwa rais wa Ufaransa. kutoa tamko lolote kuhusu uamuzi wa Alassane Ouattara kuwania katika uchaguzi wa urais ujao.

Machi 5 rais Emmanuel Macron alikaribisha tangazo la Alassane Ouattara la kutowania muhula mwingine, akimwita "mtu mwenye busara na kiongozi wa serikali mwenye hekima".

Lakini, tangu rais wa Côte d’Ivoire kubadili kauli ujao, Agosti 6, na kutangaza kuwa yuko tayari kuwania katika uchaguzi wa urais ujao, Paris imekaa kimya.Kwa hiyo upinzani nchini Côte d’Ivoire umiomba Paris kuonyesha msimamo wake.

Hivi karibuni Pascal Affi N’Guessan, ambaye ni mgombea wa chama cha upinzani cha FPI alimwandikia rais wa Ufaransa barua ya wazi akibaini kwamba tangazo la Alassane Ouattara kuwania muhula mwingine, ni "mapinduzi ya taasisi", na ni "chanzo cha mgogoro". "Alassane Ouattara anakuja kukuomba uungwaji wako mkono kwa uhalifu wake, tunataka angalau uonyeshe msimamo wako kufuatia uamuzi wake," Pascal Affi N’Guessan aliandika. "Ukimya wako (…) unatafsiriwa tofauti katika nchi yangu. Kauli yako inasubiriwa kwa hamu hapa nchini", aliongeza Waziri Mkuu wa zamani wa Côte d’Ivoire.

Na Spika wa zamanai wa nchi hiyo Guillaume Soro alimuandika barua rais wa Ufaransa akimtaka kuonysha msimamo wake kufuatia uamuzi wa Alassane Ouattara kutaka kuwania muhula mwingine.

Hata hivyo mawaziri mbalimbali wa serikali ya Côte d’Ivoire wamekuwa wakionyesha kwenye vyombo mbalimbali vya Ufaransa kuwa hatua ya Alassane Ouattara sio kinyume na katiba ya nchi.