MALI-SIASA-IBK-USALAMA

Aliye kuwa rais wa Mali aruhusiwa kuondoka hospitalini

Ibrahim Boubacar Keïta, Juni 30, 2020.
Ibrahim Boubacar Keïta, Juni 30, 2020. AFP/Ludovic Marin

Aliye kuwa rais wa Mali ibrahim Boubacar Keïta (IBK) ameruhusiwa kurudi nyumbani baada ya kulazwa hospitalini Jumanne wiki hii, familia yake imesema.

Matangazo ya kibiashara

Ndugu zake wanadai kuwa ilikuwa uchunguzi wa kawaida wa matibabu. Lakini duru za hospitali zinabaini kwamba alikuwa amepatwa na ugonjwa wa aina ya kiharusi.

Alirudi nyumbani Alhamisi jioni baada ya kuonekana kuwa hali yako haikuwa hatarini, kulingana na vyanzo vya hospitali. Ibrahim Boubacara Keita alilazwa siku mbili katika hospital Pasteur mjini Bamako.

Hata hivyo familia yake inasema kuwa aanaendelea vizuri, na amefanya vipimo vyote, na daktari wakea anaendelea kufuatialia akiwa nyumbani, familia yak imeongeza.

Wakati huo huo ujumbe wa kundi la wanajeshi waliompindua madarakani ukiongozwa na kiongozi wake, Kanali Assimi Goïta ulikwenda kumuona hospitalini. Mazungumzo yalikuwa mazuri na kundi hilo la wanajeshi lilimtakia Ibrahim Boubacar keita kupona haraka.

Duru kutoka nchini humo zinabaini kwamba huenda Ibrahim Boubacar Keita akasafirishwa nje ya nchi huko Abu Dhabi kwa uangalizi zaidi.

Duru hizo zimeongeza kwamba viongozi wa sasa wa Mali wanatarajia kutuma ndege itakayomsafirisha. Mazungumzo yanaendelea kuhusu majina ya watu kutoka familia yake watakaoongozana naye.

Ibrahim Keïta (75) alizuiliwa kwa siku kumi na wanajeshi kabla ya kutangaza kujiuzulu na baaadae kuachiliwa huru.

Wakati wa mazungumzo yakifanyika kutafuta muafaka wa mzozo wa kisiasa nchini Mali Keita alinukuliwa akisema kuwa hana haja ya mamlaka ya urais.

Ikumbukwe miezi kadhaa upinzani ulikuwa ukimshinikiza rais huyo kujiuzulu na kumlaumu kwa kurudisha nyuma uchumi wa nchi, kushindwa kudhibiti ufisadi na kukabiliana na makundi ya kigaidi.