DRC-BUNIA-USALAMA

DRC: Hali ya wasiwasi yatanda Bunia baada ya wanamgambo kuingia mjini

Moja ya maeneo ya mji wa Bunia, nchini DRC, Novemba 9, 2015.
Moja ya maeneo ya mji wa Bunia, nchini DRC, Novemba 9, 2015. AFP PHOTO/EDUARDO SOTERAS

Makumi ya wanamgambo wa CODECO wameingia katika mji wa Bunia, katika mkoa wa Ituri, leo Ijumaa asubuhi. Walikuwa wamekuja kuomba kuachiliwa huru kwa wafungwa wenzao na walibaki karibu na gereza kwa saa chache, kabla ya kuanza kuondoka.

Matangazo ya kibiashara

Mapema asubuhi wanamgambo CODECO waliingia katika wilaya za kusini mwa jiji ambako - inasemekana- kuna wafuasi wao. Wanamgambo hao walikuwa wamekusanyika karibu kilomita kumi na mj wa Bunia, walikuwa wameahidi kuweka chini silaha na walikuwa wanangojea msaada wao, kupitia mchakato wa kupokonywa silaha na kurejeshwa katika maisha ya kiraia.

Pia wamekuwa wakidai, kuachiliwa huru kwa wenzao wanaoshikiliwa katika gereza la Bunia. Hapo ndipo walikwenda leo asubuhi wakisindikizwa na vikosi vya usalama, mashahidi wamesema.

Afisa mmoja amebaini kwamba wanamgambo hao wamedanganya vikosi vya jeshi kwa kuwahakikishia kuwa wanataka kuweka chini. Haijulikani, kwa sasa, ikiwa madai yao yamepatiwa ufumbuzi. Mazungumzo na mamlaka yamefanyika, hali ambayo imepelekea waondoke karibu na gereza, vyanzo kadhaa vimethibitisha.