MALI-USALAMA

Mali: Wanajeshi kumi waangamia katika shambulio la kuvizia katikati mwa nchi

Bamako, mji mkuu wa Mali, Agosti 9, 2018
Bamako, mji mkuu wa Mali, Agosti 9, 2018 REUTERS/Luc Gnago

Mali imepoteza wanajeshi wake kumi waliouawa katikati mwa wili hii karibu na mji wa Nara, katikati mwa nchi, karibu kilomita 500 kaskazini mwa mji mkuu Bamako.

Matangazo ya kibiashara

Wauaji walitega kwanza mabomu ya ardhini kwenye barabara iliyokuwa ikitumiwa na msafara wa magari ya jeshi la Mali. Mlipuko mkubwa ulisikika, kulingana na ripoti. Kisha washambuliaji walitumia silaha zao kivita, wakilenga kwa karibu msafara huo, katika mji wa Guiré, unaopatikana katika eneo lililo karibu na mpaka wa Mauritania.

Angalau wanajeshi kumi wa Mali, ikiwa ni pamoja na afisa wa cheo cha luteni, waliuawa, magari ya jeshi yaliharibiwa na gari la wagonjwa lilitekwa nyara.

Hakuna kundi lililodai kuhusika na shambulio hilo, lakini makundi ya wanamgambo wa Kiislamu yanaripotiwa katika eneo hilo nchini Mali.