DRC-HAKI-USALAMA

DRC: Sababu za kukamatwa kwa Christian Ngoy, zahusiana na kesi ya Chebeya

Askari wakati wa kusikilizwa kesi ya Chebeya, Aprili 21, 2015 (picha ya kumbukumbu)
Askari wakati wa kusikilizwa kesi ya Chebeya, Aprili 21, 2015 (picha ya kumbukumbu) AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA

Christian Ngoy ambaye amekamatwa tangu Alhamisi, Septemba 3 huko Lubumbashi na wanajeshi na kusafirishwa siku hiyo hiyo katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa, ambapo anaendelea kuzuiliwa, anatarajiwa kufikishwa kizimbani.

Matangazo ya kibiashara

Kanali Christian Ngoy Kenga Kenga, aliyehusishwa hasa na mauaji ya wanaharakati wa haki za binadamu mwaka 2010, Floribert Chebeya na Fidèle Bazana, anatarajia kujieleza mwenyewe mbele ya mahakama ya kijeshi ya DRC.

Mbali na kumiliki silaha za kivita, anatuhumiwa pia kushirikiana na mtandao wa wahalifu katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Wakati wa kukamatwa kwake, Christian Ngoy Kenga Kenga alitishia kuita kundi lake la wahalifu wenye silaha, amethibitisha shahidi mmoja ambaye ameongeza: "Lakini, hakujuwa ni watu gani wanaomshikilia na walikuwa walijihami kwa silaha gani? "

Christian Ngoy ni mkuu wa kampuni ya usalama, Miketa, ambayo wateja wake wengi ni makampuni ya madini. Kulingana na vyanzo vyetu, kampuni hii ya usalama inamilikiwa na afisa wa juu wa jeshi la DRC, mwenye cheo cha Jenerali, na lina miliki zilaha za kivita.

Mkuu wa kikosi maarufu cha Simba

Baada ya mauaji ya Floribert Chebeya na Fidèle Bazana mwezi Juni 2010 ambayo anahusishwa, Christian Ngoy Kenga Kenga, mkuu wa kikosi maarufu cha Simba, inasemekana aliendelea na shughuli zake huko Haut-Katanga alikokuwa tangu wakati huo, kwa msaada wa viongozi kadhaa walioshirikiana naye kwa uhalifu huo.

Vyanzo kadhaa vya usalama huko Lubumbashi vinamshutumu Christian Ngoy Kenga Kenga kwa kumiliki mtandao wa wahalifu, kikosi cha wanajeshi wasiodhibitiwa wanaoonekana kama wahusika katika ongezeko la ukosefu wa usalama katika "mji mkuu wa shaba" na kungineko.