MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Hali nchini Mali kujadiliwa katika mkutano wa 57 wa ECOWAS

Wawakilishi wa CNSP, kundi la jeshi linaloshikilia madaraka nchini Mali, wakati wa mkutano na ujumbe kutoka ECOWAS Agosti 22 (picha ya kumbukumbu)
Wawakilishi wa CNSP, kundi la jeshi linaloshikilia madaraka nchini Mali, wakati wa mkutano na ujumbe kutoka ECOWAS Agosti 22 (picha ya kumbukumbu) ANNIE RISEMBERG / AFP

Wakuu wa nchi za Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi wanatarajia kukutana Jumatatu hii, Septemba 7 huko Niamey, nchini Niger. Mkutano huo utajadili kuhusu hali ya kisiasa na usalama katika eneo ukanda ho mzima, ikiwa ni pamoja na hali inayoendelea nchini Mali.

Matangazo ya kibiashara

ECOWAS imesitisha kwa muda uanachama wa Mali katika jumuiya hiyo tangu mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 18. Nchi hii kwa sasa inakabiliwa na vikwazo vilivyochukuliwa na ECOWAS.

"Tunataka kusaidia ndugu zetu wa Mali, na sio kuwabana pumzi," amesema afisa mmoja kutoka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi. Huko Niamey kuanzia Jumatatu, wakuu wa nchi wanachama wa ECOWAS watakaribisha hatua ya jeshi ya kumruhusu rais wa zamani IBK kusafiri katika Umoja wa Falme za Kiarabu kwa matibabu.

Kufanyika kwa mazungumzo ya kitaifa, ikiwa ni pamoja na duru ya kwanza ambayo imemalizika hivi karibuni nchini Mali, pia inachukuliwa kama ishara ya nia njema ya kundi la jeshi lililofanya mapinduzi.

Rais wa Cote d'Ivoire Allassane Ouattara alizungumzo kwa njia ya simu mwishoni mwa wiki hii na kiongozi wa kundi la wanajeshi hao Kanali Assimi Goïta. Kipindi cha mpito pia kilijadiliwa na wawili hao. Mazungumzo yalikwenda vizuri.

Haijafahammika ikiwa mkutano huo wa Niamey unalenga kulegeza vikwazo au kuongeza. Viongozi ndio watachukuwa uamuzi juu ya suala hilo.