MALI-IBK-AFYA-SIASA

IBK kurejea nchini Mali baada ya miezi mitatu

Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita.
Rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita. Ludovic Marin /Pool via REUTERS

Uongozi wa kijeshi nchini Mali, umetoa muda wa miezi mitatu kwa aliyekuwa rais Ibrahim Boubacar Keita kurejea nchini humo, baada ya kiongozi huyo wa zamani kusafarishwa katika nchi ya Falme ya Kiarabu kupokea matibabu, baada ya kupata kiharusi wiki moja iliyopita.

Matangazo ya kibiashara

Makanali waliompindua Keita, wamesema muda huo umekubaliwa kati yao na muungano wa nchi za Kiuchumi za Afrika Magharibi ECOWAS, unaongoza mazungumzo ya kurejeshwa kwa uongozi wa kiraia nchini humo.

Hata hivyo, mazungumzo hayo yamesusiwa na kundi la waasi la CEMA lenye makao yake Kaskazini mwa nchi hiyo.

Bwana Keita aliondolewa madarakani tarehe 18 mwezi Agosti baada ya maandamano makubwa nchini humo dhidi ya utawala wake na namna inavyoshughulikia masuala ya rushwa na usimamizi wa uchumi na mzozo kuhusu uchaguzi wa wabunge.