DRC-USALAMA

Uvamizi katika mji wa Bunia: Mchakato wa kurejesha wapiganaji katika maisha ya kiraia mashakani

Askari kutoka vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri, mashariki mwa DRC (picha ya kumbukumbu)
Askari kutoka vikosi vya jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakipiga doria katika kijiji cha Kaswara, kilomita 60 kusini magharibi mwa Bunia, katika mkoa wa Ituri, mashariki mwa DRC (picha ya kumbukumbu) REUTERS

Kisa cha wanamgambo kuingia katika mji mkuu wa Mkoa aw Ituri, Bunia, siku ya Ijumaa, kimeibua maswali mengi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Matangazo ya kibiashara

Wanamgambo hao waliondoka msituni na kuandamana mbele ya makao makuu Mkoa, kudai kuachiliwa huru kwa wenzao, lakini pia huduma bora kutoka kwa serikali.

Baada ya majadiliano na maafisa wa kisiasa na kijeshi, wanamgambo hao walikubaliana kurejea msituni. Hali hii inatia wasiwasi, lakini pia inahoji juu ya sula ala mchakato wa kurejesha wapiganaji katika maisha ya kiraia au kuingizwa katika idara za usalama wa nchi.

Miongoni mwa maswali ambayo yameibuka, kuna yale ya ufadhili wa wanamgambo wa Codeco. Wabunge wengine wanahoji kuhusu kuendelea kuepo kwa kundi hili na kuendelea kukabiliana na jeshi lenye nguvu na polisi.

Katikati mwa mwaka 2019, Félix Tshisekedi alijiuliza swali hilo, na kuhitimisha kwamba "bila msaada wa ziada, wanamgambo hawangelikuwa jinsi walivyo hivi leo". Miezi kadhaa baadaye, swali hili bado halijajibiwa.

Swali lingine ni lile la kuzindua kampeni ya kuhimiza na mazungumzo inayoongozwa na viongozi wa zamani wa vita, bila kuepo kwa tume yenye dhamana ya kuwarejesha wapiganaji katika maisha ya kiraia na kuwaingiza katika idara za usalama na jeshi ( DDR).

Tayari mwezi Januari, kampeni kama hiyo ilifanywa. Zaidi ya wapiganaji 200 walijisalimisha, lakini baadaye walirudi msituni, kutokana na kukosekana kwa ufuatiliaji mzuri katika kambi walikokusanywa.