DRC-BUNIA-HAKI

Wafungwa wa jela kuu la Bunia waishi katika mazingira magumu

Bunia, mji mkuu wa Ituri.
Bunia, mji mkuu wa Ituri. AFP PHOTO/EDUARDO SOTERAS

Wafungwa katika Gereza la Bunia mkoani Ituri, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanakabiliwa na baa la njaa, baada ya wawili kufafiki dunia wiki iliyopita kutokana na hali hiyo na kufanya idadi kufikia 17 tangu mwezi Aprili.

Matangazo ya kibiashara

Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, yanasema mamia ya wafungwa hupoteza maisha kila mwaka katika mazingira kama hayo.

Duru za kuaminika znabaini kwamba wafungwa katika gereza la Bunia wana ukosefu mkubwa wa chakula na pia wanakosa huduma ya matibabu.

"Hatuna chakula, hatuna dawa na hata pia mahali pa kulala. Tunapewa tu kikombe kimoja cha uji na hiyo baada ya masaa 72, " amesema mmoja wa wafungwa hao ambaye hakutka kutaja jina lake.

Kulingana na Meja Camille Nzonzi, kiongozi wa gereza la Bunia, hali hii inasababishwa na  serikali.

"Tangu Januari, hatujapokea pesa yoyote kutoka kwa serikali. Na leo, tunaweza kukwambia kuwa hakuna chochote katika amana yetu, hatuna chakula na hii kwa wiki moja sasa . Kwa siku nne, wafungwa hawajapata chochote cha kula. Hivi karibuni wafungwa wawili walifariki, " amesema kiongozi wa gereza la Bunia.

"Mbali na hayo,kuna ukosefu wa dawa, tuna madaktari lakini hawajui tena kutibu wagonjwa. Wagonjwa hapa gerezani wanabaki bila msaada wowote, " ameongeza Meja Camille Nzonzi

Mbali na uhaba wa chakula, gereza kuu la Bunia linakabiliwa na msongamano wa wafungwa,  hiyo ikiwa hali inayozikabili gereza kadhaa inchini DRC.Gereza kuu la Bunia, ambalo lina uwezo wa kupokea wafungwa 220, sasa lina zaidi ya 1,300,  ikiwa ni mara sita zaidi.