NIGER-MAJANGA ASILI

Niger: Niamey yakumbwa na mafuriko baada ya mvua kubwa kunyesha

Mji wa Niamey wakumbwa na maji baada ya mvua kubwa ku,yesha, Niger, Agosti 27, 2020.
Mji wa Niamey wakumbwa na maji baada ya mvua kubwa ku,yesha, Niger, Agosti 27, 2020. BOUREIMA HAMA / AFP

Mji mkuu wa Niger, Niamey, umekumbwa na mafuriko ya kihistoria kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha katika jiji hilo. Maji yamepanda kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa.

Matangazo ya kibiashara

Mvua zilizonyesha katika siku za hivi karibuni zimesababisha mabwawa kuvunjika, na kusababisha uharibifu mkubwa katika mashamba ya mpunga na kuharibu maelfu ya nyumba.

Hospitali ya kitaifa ya Lamordé, iliyokuwa ikiitwa zamani CHU, imejaa maji. Rais Mahamadou Issoufou almezuru eneo hilo leo Jumanne asubuhi.

Maji ya Mto Niger yanaendelea kusababisha madhara katika ukingo wa kulia wa mto. Kwa kipindi cha saa 48, wakazi wa Saga, Lamordé, Nogare na maeneo jirani hawajui wapi pakukimbilia. “Kwa hiyo ni baada ya saa zisizozidi mbili, tulijikuta tumekumbwa na mafuriko. Nimekuwa katika eneo hili tangu mwaka 1974 ”, mkazi mmoja amebaini.

Kwa karibu miaka 60, kiasi kama hicho cha mvua hakijanyesha katika mwambao huo wa Niamey, amesema Aliza Abdou mmoja wa wakazi wa maeneo hayo.

"Tangu nizaliwe, sijawahi kuona maajabu haya. Hii ni mara ya kwanza kuona maji yakitufunika hapa kwenye eneo letu" , ameongeza