SOMALIA-USALAMA

Somalia yawapoteza wanajeshi wake watano katika shambulio

Somalia imeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kundi la Al Shabab.
Somalia imeendelea kukabiliwa na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kundi la Al Shabab. REUTERS/Feisal Omar

Wanajeshi watano nchini Somalia wameuwa na mshauri wao, raia wa Marekani amejeruhiwa baada ya kushambuiwa na kundi la kigaidi la Al Shabab.

Matangazo ya kibiashara

Mlipuaji wa kujitoa mhanga kutoka kundi hilo, akiwa ndani ya gari lenye vilipuzi, alijilipua kwenye lango la kambi ya kijeshi katika eneo la Janay Abdalla, Kusini mwa mji wa Kismayo.

Mohamed Abdulle, afisa wa usalama katika eneo hilo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo siku ya Jumatatu na juhudi za kuzuia shabbulizi hilo halikufua dafu.

Kundi la Al-Shabab limekiri kutekeleza shambulizi hilo na kudai kuwa limewauwa wanajeshi 16 wa Somalia na wengine wanne kutoka Marekani.

Hata hivyo, madai ya Al Shabab hayawezi kuaminika kwa sababu mara kwa mara linaongeza idadi katika mashambulizi yake.

Mwezi Uliopita, watu 10 waliuawa baada ya kundi hilo kushambulia hoteli moja kwenye ufukwe wa bahari Hindi jijini Mogadishu.

Somalia imekosa amani kwa miaka zaidi ya 30 sasa, na tangu mwaka 2008 serikali jijini Mogadishu imekuwa ikipambana na kundi la Al Shabab.