SUDA-MAFURIKO-MAJANGA ASILI

Sudan: Mafuriko mabaya yasababisha zaidi ya watu 500,000 kutoroka makazi yao

Mafuriko ya awali huko Khartoum, Sudan.
Mafuriko ya awali huko Khartoum, Sudan. Ebrahim Hamid / AFP

Nchini Sudan raia wamekwama katika maeneo yenye mafurikio tangu mwishoni mwa mwezi Julai kutokana na mafuriko ya Mto Nile huko Mashariki na mvua kubwa Magharibi.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka za mitaa zimetangaza hali ya dharura ya miezi mitatu na kuhamasisha jeshi wakati maji yanayopanda tayari yameua karibu watu 100, na kuharibu nyumba zaidi ya 100,000 na kusababisha zaidi ya nusu milioni ya wakazi kuyatoroka makazi yao.

“Kwa watu walioyahama makazi yao, baadhi wanaweza kupewa hifadhi kwa marafiki wao au familia lakini wengi huishi katika makambi au katikamahema au katika majengo ya serikali kama shule, lakini shule zinatarajiwa kufunguliwa katika wiki zijazo. Kipi kitakachotokea? Hatuwezi kuwatimua, lakini shule zinapaswa kufunguliwa. Kwa kuongezea, shule zingine zimekumbwa na mafuriko tena, vipi tutaandaa mwanzo wa mwaka wa shule? Pamoja na maji kuongezeka, pia kuna tatizo la magonjwa kama malaria na hasa kipindupindu au hata nyoka na nge ambao wamelazimika kukimbilia maeneo salama na wanaweza kuuma watu wengi zaidi, na kwa hali hiyo huduma haitolewi kila kwa wakati. Haya yote ni mambo ambayo tunapaswa kushughulikia hivi sasa na bila kusahau kuwa yanaweza hata kushughulikiwa baadaye, kwa sababu hiyo ni muhimu sana", amesema Tanogo Chikoto, kutoka Ofisi ya Umoja wa mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu, OCHA, katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati (OCHA) huko Khartoum.