ETHIOPIA-SIASA-USALAMA

Ethiopia: Wakazi wa jimbo la Tigray wapiga kura

Jimbo la Tigray nchini Ethiopia (picha ya kumbukumbu)
Jimbo la Tigray nchini Ethiopia (picha ya kumbukumbu)

Leo Jumatano ni siku ya uchaguzi nchini Ethiopia, lakini uchaguzi huo unafanyika katika jimbo la Tigray pekee, kaskazini mwa nchi hiyo, mpakani na Eritrea.

Matangazo ya kibiashara

Serikali ya mkoa, katika mgogoro wa wazi na mamlaka ya shirikisho ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed, imeamua kufanya uchaguzi wa wabunge katika hali yoyote ile, ikitoa ikijitetea kwamba kuahirishwa rasmi kwa uchaguzi katika ngazi ya kitaifa kwa sababu ya ugonjwa wa Covid-19 ni 'kisingizio' cha waziri mkuu kubaki madarakani.

Tigray inaingia leo Jumatano katika sintofahamu. Kwa miezi kadhaa, mamlaka ya shirikisho, ikiwa ni pamoja na Waziri Mkuu Abiy Ahmed mwenyewe au tume ya kitaifa ya uchaguzi, walitaka uchaguzi wa Septemba 9 usifanyike. Wanalaani zoezi "lisilo la kikatiba" na kutishia "kuiadhibu" serikali ya jimbo la mkoa wa waasi.

Huko Mekele na katika vijiji vya Tigray, wanapiga kura leo Jumatano. Vyama vichache vya kisiasa vinashiriki uchaguzi huo kuwachagua wabunge wao. Chama cha Ukombozi cha Watu wa Tigray (TPLF), ambacho kilitawala Ethiopia tangu kuanguka kwa Mengistu hadi kuingia madarakani kwa Abiy Ahmed mmwaka 2018. Na vyama viwili vya kitaifa, ambavyo vitatazamwa kwa karibu, kwani vina msimamo mkali zaidi kuliko chama cha TPLF juu ya swali la uwezekano wa uhuru wa Tigray.

Jibu la Addis Ababa linapaswa kuwa kutotambuliwa kwa uchaguzi huu na bila shaka kuzuiwa kwa mapato ya shirikisho huko Tigray, ambayo yanawakilisha nusu ya bajeti ya jimbo hilo. Hivi karibuni Abiy Ahmed alisema kuwa uingiliaji wa kijeshi kuzuia uchaguzi huo itakuwa "upumbavu", kauli ambayo maafisa wengine wakuu wa jeshi la shirikisho wanasema hawakubaliani nayo.