SUDA-SIASA-USALAMA-AMANI

Hatma ya Sudan kujulikana baada ya utiaji saini wa mkataba wa mwisho wa amani Oktoba 2

Mkataba huo umetiwa saini kati ya  serikali na muungano wa makjundi matano ya waasi na vyama vinne vya upinzani kutoka majimbo la Darfur, Korodopfan Kuisni na Blue Nile.
Mkataba huo umetiwa saini kati ya  serikali na muungano wa makjundi matano ya waasi na vyama vinne vya upinzani kutoka majimbo la Darfur, Korodopfan Kuisni na Blue Nile. RFI/Stéphanie Braquehais

Raia wa Sudan wanasubiri utiaji saini wa mkataba wa mwisho wa amani tarehe 2 mwezi Oktoba, kati ya waasi na serikali ya Khartoum, lakini swali kubwa ni iwapo mkataba huo utadumu na kurejesha amani ya kudumu.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakuja baada ya serikali ya Sudan na waasi hivi karibuni kukubaliana kumaliza mapigano ya muda mrefu ambayo yamesababisha vifo vya maefu ya watu.

Makubaliano ya awali yalitiwa saini na pande zote mbili tarehe 31 mwezi Agosti na kuleta matumaini makubwa ya mwamko mpya kuelekea utiaji saini wa mwisho mapema mwezi Oktoba.

Mkataba huo umetiwa saini kati ya serikali na muungano wa makundi matano ya waasi na vyama vinne vya upinzani kutoka majimbo ya Darfur, Korodopfan Kusini na Blue Nile.

Kikubwa kwenye mkataa huo ni ugawaji sawa wa rasilimali na madaraka lakini pia upatikanaji wa haki kwa wale waliotahirika na mauaji hayo ya muda mrefu.