DRC: Ubelgiji yatangaza kurejesha jino la Patrice Lumumba kwa familia yake
Imechapishwa:
Mahakama ya Ubelgiji imejibu vyema ombi kutoka kwa familia ya Patrice Lumumba ya kurudisha jino la kiongozi huyo wa Congo aliyeuawa mwezi Januari 1961 nchini humo, Ofisi ya Mashtaka nchini Ubelgiji imeliambia leo Alhamisi shirika la habari la AFP.
Jino hilo lilikamatwa kutoka kwa familia ya polisi wa Ubelgiji ambaye alichangia kwa kupoteza mwili - ambao haujapatikana - wa yule ambaye alikuwa Waziri Mkuu wa muda wa katika koloni la zamani la Ubelgiji baada ya nchi hiyo kupata uhuru Juni 30, 1960.
Jino hilo ni moja ya vielelezo vya faili ya kimahakama iliyofunguliwa baada ya malalamiko yaliyowasilishwa mwaka 2011 huko Brussels na watoto kadhaa wa Patrice Lumumba, wakitaka mazingira ya mauaji ya baba yao yawekwe wazi. Jino hilo sasa "litarejeshwa kwa walengwa" wa Patrice Lumumba, Eric Van Duyse, msemaji wa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka nchini ubelgiji ameliambia shirika la habari la AFP.
Amebaini kwamba kurejeshwa kwa jino hilo ni "ishara" baada ya kutokuwa na "uhakika wa kutosha" kwamba jino hilo kweli lilikuwa la shujaa wa uhuru. "Hakukuwa na vipimo (DNA) kwenye jino, kwani vipimo hilo vingeliharibu," amesema Van Duyse.
Mwaka 2000, afisa wa polisi wa Ubelgiji Gérard Soete alikubali kutoa ushahidi kwa shirika la habari la AFP juu ya ushiriki wake, miaka 40 karibu, baada ya kupotezwa mwili wa Lumumba, aliyeuawa yeye na wasaidizi wake wawili katika mkoa wa Katanga ambao wakati huo uliokuwa ulijitenga, karibu na mji wa Elisabethville, Lubumbashi ya leo.