MALI-SIASA-USALAMA

Mali: Jeshi laendelea kukutana kwa minajili ya kupatikana suluhu ya mzozo unaoendelea

Kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Mali wakisherehekea mapinduzi waliofanya.
Kundi la wanajeshi waliofanya mapinduzi nchini Mali wakisherehekea mapinduzi waliofanya. REUTERS/Mamadou Keita

Wanajeshi walioipindua serikakali ya Mali wanakutana na mamia ya wadau mbalimbali wa kitaifa kwa mara nyingine siku ya Alhamisi kujaribu kutafuta suluhu ya mzozo wa baada ya mapinduzi hayo, wakati huu wanapoendelea kupata shinikizo za kuunda serikali ya kiraia.

Matangazo ya kibiashara

Washiriki wengine 500, viongozi wa vyama vya kisiasa, vyama vya wafanyakazi, asasi za kiraia, wanatarajiwa kukutana kuanzia mapema  Alhamisi hadi Jumamosi katika "siku hizi za mashauriano ya kitaifa"

Mara tu baada ya kumpindua rais Ibrahim Boubacar Keïta, wanajeshi waliokusanyika karibu na Kanali Assimi Goïta waliahidi kupeana udhibiti kwa raia baada ya kipindi cha mpito, cha asili (raia au kijeshi) na shirika litakaloamuliwa. Sasa ni suala la kukubaliana juu ya kipindi hicho cha mpito.

Lakini hata hivyo mwezi mmoja baada ya mapinduzi hayo ambayo ni ya mara nne kushuhudiwa nchini humo tangu uhuru wake mwaka 1960, na licha ya kikao cha kwanza cha mashauriano Jumamosi, hakuna mabadiliko yoyote yanayoshuhudiwa.

Wananchi wa Mali walipongeza hatua ya mapinduzi  na walikasirishwa kuona nchi yao kubwa ikizama chini ya athari ya vita dhidi ya makundi ya kijihadi, ghasia za kijamii, kudorora kwa uchumi na ukosefu wa nguvu za serikali, huku mizozo ikiongezeka.