MALI-USALAMA

Mali: Wanajeshi wanne wa Mali wauawa katika shambulio

Wanajeshi wa Mali (FAMA) wakipiga doria katika mitaa ya huko Anderamboukane, katika mkoa wa Menaka, mnamo Machi 22, 2019.
Wanajeshi wa Mali (FAMA) wakipiga doria katika mitaa ya huko Anderamboukane, katika mkoa wa Menaka, mnamo Machi 22, 2019. Agnes COUDURIER / AFP

Wanajeshi wanne wa Mali wameuawa katika shambulio lililotokea katikati mwa nchi hiyo Jumarano wiki hii. Wanajeshi hao waliuawa katikati mwa Mali, moja ya maeneo makuu yanayokabiliwa na machafuko mabaya tangu miaka kadhaa nchi hiyo ikiwa katika vita, kulingana na vyanzo vya usalama.

Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo lilitokea karibu na Alatona, sio mbali na mji wa Niono, shirika la habari la AFP limenukuu taarifa kutoka Wizara ya Usalama na serikali ya eneo hilo.

Wakati huo huo Imam Mahmoud Dicko, kiongozi wa kidini mwenye ushawishi mkubwa nchini Mali ametoa wito kwa viongozi wa jeshi kutekeleza amri ya viongozi wa jumuiya ya Afrika Magharibi ya kumteua rais na waziri mkuu kufikia septemba 15 ili kulegeza vikwazo vilivyowekwa mwezi uliopita.

Hapo jana, Dicko ameliambia shirika la taifa la habari kwamba nchi hiyo inahitaji usaidizi na kwamba haifaidiki na chochote kwa kwenda kinyume na jamuiya kimataifa.