MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Wataalam: Kipindi cha mpito cha miaka miwili nchini Mali ni mihimu kwa usalama wa nchi

Ismael Wague, the spokesperson for the CNSP (National Committee for the Salvation of the People) arrives at the CNSP headquarters on the military base in Kati, Mali, just outside of Bamako, for a meeting with M5-RFP leaders on August 26, 2020.
Ismael Wague, the spokesperson for the CNSP (National Committee for the Salvation of the People) arrives at the CNSP headquarters on the military base in Kati, Mali, just outside of Bamako, for a meeting with M5-RFP leaders on August 26, 2020. © Annie Risemberg/AFP

Wataalam wa sheria za katiba wanapendekeza kipindi cha mpito cha miaka miwili nchini Mali baada ya mapinduzi ya kijeshi ya Agosti 18, licha ya ombi la viongozi wa nchi za Afrika Magharibi kutaka uchaguzi ufanyike baada ya kipipindi cha mpito cha mwaka mmoja.

Matangazo ya kibiashara

Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS), baada ya kutaka Mali kuwa mfano katika eneo hilo, ilichukua haraka vikwazo dhidi ya wanajeshi waliompindua rais Ibrahim Boubacar Keïta Agosti 18 na kutaka wanajeshi hao wanaoshikilia madaraka kumteua rais na waziri mkuu wa mpito ifikapo Septemba 15 kabla ya uchaguzi ambao unatakiwa kufanyika katika kipindi cha miezi 12.

Wakati wa siku ya pili ya mashauriano yaliyofanyika katika mji wa Bamako kuhusu kipindi hiki cha mpito, wataalam hao sheria za katiba wameandika katika waraka wa kurasa nane, uitwao "Hati ya Mpito", kwamba kipindi cha miezi 24 kingelikuwa muhimu kabla ya uchaguzi mpya " kutokana na utata, hali inayojiri na ukubwa wa mgogoro wa Mali ".

Wametoa mapendekezo kwa kundi la wanajeshi wanaoshikilia madaraka, kumteua rais na makamu wa rais wa mpito na kupendekeza mgombea kwenye nafasi ya waziri mkuu, ambaye atateuliwa na kaimu rais mteule.

Mapendekezo haya bado hayajaidhinishwa rasmi na wawakilishi wa Kamati ya Kitaifa ya Uokovu wa Wananchi (CNSP). Mashauriano yanatarajiwa kumalizika Jumamosi.

Wakati ECOWAS na viongozi wengine wa Mali wanasisitiza kwamba wadhifa wa rais wa mpito apewe raia, waraka wa wataalam unabaini kwamba askari anaweza pia kuchukua wadhifa huo.

Wagombea kwenye wadhifa huo wanapaswa wawe na umri kati ya miaka 35 na 75 na hawataweza kugombea katika uchaguzi wa urais mwishoni mwa kipindi cha mpito, hati hiyo imsema.