DRC-USALAMA

Hamsini wafariki dunia kwa kuangukiwa na mgodi wa dhahabu DRC

Jamhuri ya Kidemekrasi ya Congo ni nchi tajiri kwa dhahabu, almasi na coltan lakini migodi mingi inadhibitiwa na makundi yenye silaha.
Jamhuri ya Kidemekrasi ya Congo ni nchi tajiri kwa dhahabu, almasi na coltan lakini migodi mingi inadhibitiwa na makundi yenye silaha. REUTERS/Pete Jones

Takriban watu 50 wanadaiwa kufariki dunia baada ya kuangukiwa na kifusi cha udongo katika mgodi wa dhahabu karibu na eneo la Kamituga mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, shirika moja lisilo la kiserikali katika eneo hilo limesema.

Matangazo ya kibiashara

"Wachimbaji kadhaa walikuwa kwenye kisima ambacho kilifunikwa na udongo na hakuna mtu aliyeweza kuokolewa. Idnadaiwa kuwa vijana hamsini ndio walikuwa katika shimo hilo la mgodi," amesema Emiliane Itongwa, kiongozi wa shirika moja la wanawake.

Mkasa kama huo hutokea mara nyingi katika nchi mbalimbali duniani, na watu wameekuwa wakipoteza maisha kutokana na hali hiyo.

Jamhuri ya Kidemekrasi ya Congo ni nchi tajiri kwa dhahabu, almasi na coltan lakini migodi mingi inadhibitiwa na makundi yenye silaha.

Watu wa DRC ni miongoni mwa watu maskini zaidi barani Afrika ingawa nchi hiyo ni tajiri kwa rasilimali.

Mashariki mwa DRC kumekuwa na migogoro kwa karibu miaka 24 sasa, huku wote jeshi na makundi ya waasi yakituhumiwa kutumia mapigano kama kisingizio wakati vikichota utajiri wa madini katika eneo hilo.

Wachambuzi wanasema soko la kimataifa kwa madini ya Coltan ni mojawapo ya vyanzo vya mgogoro na kuwepo kwa wanamgambo nchini humo.

Mwezi Mei 2011 serikali iliondoa kizuizi kwenye machimbo ya mashariki, eneo lililoathiriwa zaidi na migogoro ya DRC ya muda mrefu.

Makampuni ya kigeni ndio wawekezaji wakubwa nchini DRC.