DRC-FRPI-USALAMA

Mchakato wa kuwapokonya silaha waasi wa FRPI wakwama DRC

Aveba, katika mkoa wa Ituri, DR Congo: Kamanda wa kikosi cha MONUSCO kutoka Bangladeshi, akiongozana na mkuu wa operesheni, wakiwa  pamoja na wanajeshi katika mkoa wa BUKIRINGI-AVEBA wakati wa operesheni "UPPERCUT" dhidi ya wanamgambo wa FRPI.
Aveba, katika mkoa wa Ituri, DR Congo: Kamanda wa kikosi cha MONUSCO kutoka Bangladeshi, akiongozana na mkuu wa operesheni, wakiwa pamoja na wanajeshi katika mkoa wa BUKIRINGI-AVEBA wakati wa operesheni "UPPERCUT" dhidi ya wanamgambo wa FRPI. Photo MONUSCO/Force

Wakazi wa mkoa wa turi, Kaskazini Mshariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wameendelea kuwa na wasiwasi na hali inayojiri katika mkoa huo, baada ya kukwama kwa mchakato wa kuwarejesha waasi wa FRPI katika maisha ya kiraia.

Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa mwezi wa Februari, kundi la waasi la FRPI lilitia saini mkataba wa amani uliyoelezewa kama "wa kihistoria" na serikali ya Congo. Monusco na washirika mbalimbali walikuwa mashahidi, na walikaribisha maendeleo katika mchakato wa amani katika mkoa huo wa Ituri. Tangu wakati huo, mchakato huo umekwama na wakazi wanahofu kwamba wanamgambo huenda wakarejeshea msituni.

Pamoja na mkataba huo wa amani, ratiba ya DDR (tume ya mseto inayohusika na kuwapokonya silaha na kuwarejesha wapiganaji wa zamani katika maisha ya kiraia na wengine kuingizwa katiika idara za usalama na ulinzi) ilipitishwa. Na zoezi la kuwapokonya silaha waasi hao lilitarajiwa kuanza mapema mwezi Mei. Tangu wakati huo, hakuna kilichofanyika. Wanamgambo wenye silaha bado wako Azita, karibu kilomita 10 kutoka mji wa Gety, katika eneo la Irumu. Vyanzo kadhaa vinabaini kwamba wanamgambo wengi wametoroka eneo hilo, kwa sababu, wanasema, pesa na chakula kilichotolewa mwanzoni mwa mwaka na serikali hakijafika tangu mwezi Juni.

Kwa upande wake, tume ya Umoja aw Mataifa nchini DRC, MONUSCO, inabaini kwamba imeweka maeneo ya ambako watapokelewa wanamgambo hao, lakini ujumbe huo wa Umoja wa Mataifa kwanza unaomba waasi hao kupokonywa silaha ili kuweza pia kuweka mchakato wa kuwaingiza katika idara za usalama na ulinzi. Vyanzo vya serikali vinashutumu kundi la FRPI kwa kuleta madai mapya ambayo hayakuwa kwenye mkataba.

Kutokana na hali hii, Kinshasa sasa inapanga majadiliano kamili ili kushirikisha makundi yote yenye silaha katika mkoa huo. Ujumbe wa wa serikali uliowasili Ituri siku ya Alhamisi unaweza kusaidia kusuluhisha mzozo huo.