MALI-ECOWAS-SIASA-USALAMA

Kipindi cha mpito nchini Mali: Jeshi lajiandaa kukutana na ECOWAS nchini Ghana

Mji mkuu wa Ghana, Accra.
Mji mkuu wa Ghana, Accra. Creative Commons/Guido Sohne

Wanajeshi walioko madarakani nchini Mali wanajiandaa kukutana na wakuu wa nchi jirani. Marais wa Jumuiya ya Kiuchumi ya nchi za Afrika Magharibi, ECOWAS, wanatarajia kukutana Jumanne hii, Septemba 15 huko Accra, nchini Ghana.

Matangazo ya kibiashara

ECOWAS ilikuwa imetoa muda kwa kundi la wanajeshi wanaoshikilia madaraka nchini Mali hadi Sptemba 15 wawe wamekabidhi mamlaka kwa raia, lakini mashauriano ya kitaifa yanatofautiana na ombi hili.

Ndege iliyokodishwa na Ghana inatarajiwa kuwasili katika mji mkuu wa Mali, Bamako, Jumatatu hii, Septemba 14, kwa minajili ya kusafirisha ujumbe kutoka Mali. Huenda kiongozi wa kundi la wanajeshi hao, Kanali Assimi Goïta, akashiriki mkutano. Itakuwa safari yake ya kwanza nje ya nchi baada ya jaribio la mapinduzi lililomtimuwa mamlakani rais Ibrahim Boubacar Keita, Agosti 18.

Kulingana na wale walio karibu naye, safari hii ni muhimu: hakuna haja ya kwenda kukabiliana na marais wa Jumuiya ya Kiuchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi.